Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
WANAFUNZI wa vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na WANAFUNZI wa kidato cha sita watarejea masomoni ifikapo tarehe 1/6/2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza leo Mei 21, 2020 kwenye Ikulu ya Chamwino nje kidogo ya jiji la Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua hivi karibuni.
Serikali ilitangaza kufunga vyuo na shule zote kuanzia zile za awali miezi miwili iliyopita kufuatia kuripotiwa kisa cha kwanza cha mtu aliyeambukizwa virusi vya Korona vinavyosababisha homa Kali ya mapafu.
Aidha Rais amesema WANAFUNZI wa shule za awali, msingi na zile za sekondari ukiondoa wale wa kidato cha sita watasalia majumbani ili serikali ijipe muda wa kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa huo wa Covid-19 kabla ya kuwaruhusu na wao kurejea shuleni.
Rais pia ameruhusu michezzo agufulinayo kufunguliwa ifikapo tarehe 1/6/2020 na kuiagiza Wizara ya Afya Maendeleo utya kuratibuJqmii Jinaia, Wazee na Watoto kwa aratibukuwhirikiana na ile ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuweka utaratibu maalum kwa Wanamichezo wa Michezo inaporejeahiyo ikiwemo ya ligi za soka.
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha leo tarehe 21 Mei 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha leo tarehe 21 Mei 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Generali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.
Viongozi walioapishwa na Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Dkt. Delphine Magere-RAS Pwani, Jacob Kingu-Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Phaustine Kasike Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi John Simbachawene Balozi wa Tanzania nchini Kenya pamoja na Brigedia General John Mbungo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Viongozi mbalimbali aliowaapisha Wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020. PICHA NA IKULU
Viongozi walioapishwa na Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Dkt. Delphine Magere-RAS Pwani, Jacob Kingu-Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Phaustine Kasike Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi John Simbachawene Balozi wa Tanzania nchini Kenya pamoja na Brigedia General John Mbungo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Viongozi walioapishwa na Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Dkt. Delphine Magere-RAS Pwani, Jacob Kingu-Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Phaustine Kasike Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi John Simbachawene Balozi wa Tanzania nchini Kenya pamoja na Brigedia General John Mbungo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

No comments:
Post a Comment