Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiongea na waandishi wa habari akielezea kwa namna gani wanavyofanikiwa kutunza mazingira.
Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiongea na waandishi wa habari akielezea kwa namna gani wanavyofanikiwa kutunza mazingira.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
ZAIDI ya miche ya miti milioni moja hugawiwa kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya misitu na wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema lengo la kutoa miche hiyo kuendelea kuchukua hatua madhubuti za ulinzi shirikishi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuondosha hatari zitokanazo na uharibifu wa mazingira
Alisema kuwa Jamii Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya binadamu.
Alisema ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku akitaja za kutoweka kwa bayoanuai
Mwita alieleza namna ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo ajira na ufugaji wa nyuki.
Alisema kuwa misiti imekuwa na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.
“Umeme unazalishwa katika vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema
Alisema upandaji wa miti unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote ulimwenguni.
Aidha Mwita alisema kuwa shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.
Kwa upande mdau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill Alex Kalinga alisema kuwa wamekuwa wananufaika na uwepo wa miti pamoja na kupewa elimu ya uhifadhi wa miti.
Nao wadau wa mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonukaika na uwepo wa shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya ulinzi wa mazingira.
meneja wa Kampuni ya uzalishaji na usafirisha wa magogo na nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprises Ntibwa Mjema wamesema utunzaji wa mazingira ni matokeo chanya ya ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Mufindi na watu wake.
“kuchukua hatua za ulinzi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuendelea kunufaika na rasilimali zitokanazo na uhifadhi” Alisema Mjema
Siku ya Mazingira Duniani ni siku inayotambulika zaidi ya kushughulikia mazingira. Tangu mwaka wa 1974, imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni; ikileta pamoja serikali, mashirika ya biashara, watu maarufu na wananchi kushughulikia masuala nyeti ya mazingira.
No comments:
Post a Comment