Advertisements

Wednesday, September 23, 2020

TANZANIA NA UJERUMANI KUENDELEZA USHIRIKIANO KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Ilani ya CCM 2020/25 Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dkt. Tulia A. Mwansasu kwenye mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM zilizofanyika katika Uwanja wa CCM Ruanda Nzove Jijini Mbeya Mkoani Mbeya leo Septemba 22,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na wawakilishi kutoka ubalozi wa Ujerumani (hawapo pichani) wakati walipotembelea ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Ujerumani wakifuatilia mazungumzo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo(hayupo pichani)wakati walipotembelea ofisi za wizara zilizopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Maendeleo katika Ubalozi wa Ujerumani Dkt. Katrin Bornemann mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika ofisi za Wizara Mtumba – Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Ujerumani mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Serikalini ya Tanzania na Ujerumani wamekubalina kuendeleza mashirikiano kwenye elimu ya juu, Ufundi na Msingi ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata ujuzi wa kuweza kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wawakilishi kutoka ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kilichofanyika katika Ofisi za wizara Jijini Dodoma Katibu Mkuu Dkt Leonard Akwilapo amesema kwa sasa nchi inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hivyo kuna uhitaji wa wataalamu wenye ujuzi katika eneo.

“Tunajenga reli ya kisasa ya umeme SGR, madaraja na ipo miradi mingine mikubwa inatekelezwa, pamoja na kwamba tunao wataalamu wetu nchini bado tunahitaji wajiendeleze ili kupata ujuzi zaidi. Kwa hiyo tumezungumza nao kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kuwezesha mafunzo kwa Vijana hapa nchini na hata nchini kwao,” aliongeza Dkt. Akwilapo.

Akizungumzia uimarishaji wa elimu ya Msingi Katibu Mkuu Akwilapo amesema wamekubaliana kushirikiana kuongeza ujuzi wa walimu katika mbinu mpya za ufundishaji ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya kufundishia.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Maendeleo katika Ubalozi wa Ujerumani nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema Serikali ya Ujerumani itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu ambao wamekuwa nao katika elimu ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanaendelea kupata Elimu bora.

Ushirikiano wa Tanzania na Ujerumani ni wa muda mrefu kuanzia miaka ya 80 na 90 ambapo kupitia shirika lake la DAAD waliweza kutoa ufadhili wa masimo kwa wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments: