ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 10, 2022

OFISI YA RAIS UTUMISHI YAVISHIRIKISHA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUBORESHA MFUMO MPYA WA KUPIMA UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha ofisi yake na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi jijini Dodoma kilichoandaliwa kwa lengo la kupata maoni ya wadau yatakayoboresha mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa watumishi wa Umma (Public Employees Performance Management Information System-PEPMIS) ambao utaanza kutumika rasmi kuanzia mwezi Julai, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha ofisi yake na viongozi hao, kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kupata maoni ya kuboresha mfumo mpya wa usimamizi wa utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye, Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi wakifuatilia mada kuhusu mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa watumishi wa Umma utakaoanza kutumika rasmi Serikalini kuanzia mwezi Julai, 2022.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye, Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifunga kikao kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi jijini Dodoma, kilichoandaliwa kwa lengo la kupata maoni ya wadau yatakayoboresha mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa watumishi wa Umma utakaoanza kutumika rasmi Serikalini kuanzia mwezi Julai, 2022.

 

No comments: