ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 9, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA MDAHALO WA KITAIFA WA KUMBUKIZI YA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

 
 Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wananchi wa Pwani katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua Vitabu 3 vya Hayati Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Chemichemi ya fikra za Kimapinduzi, Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama cha Mapinduzi na Development as Rebellion.
 Rais Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyepokea kwa niaba ya Familia yake katika Kumbukizi ya miaka 100 iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere - Kibaha.
 Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Abdulrahman Kinana , wakiwasili katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi mbalimbali.


 

No comments: