Na Fredy Mgunda,Iringa.
MIRADI
ya maendeleo yenye thamani ya Jumla ya sh. 93.1 bilioni imetekelezwa
katika Wilaya ya Iringa Kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu Serikali ya
Awamu ya Sita ilipoingia madarakani.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo Akizungumza na wazee Pamoja na
viongozi wa dini wa Wilaya hiyo Mkoani Iringa alisema kiasi hicho Cha
fedha kilielekezwa katika miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu,
miundombinu ya barabara, maji na umeme.
Katika
kikao hicho Mkuu wa Wilaya alisema Serikali iliyochini ya Rais Samia
Suluhu Hassan katika kuhakikisha wazee wanapata unafuu wa Matibabu Bure
Jumla ya Wazee 793 wamepatiwa vitambulisho ili kuwaondoshea Changamoto
ya matibabu.
Moyo
alisema kuwa Sh 93.1 bilioni zimetumika katika miradi mbalimbali ya
maendeleo wilayani Iringa ikiwemo ujenzi wa barabara ya Kihesa Kilolo –
Igumbilo itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari mjini.
Alisema kwa sasa magari yote yanapita katikati ya mji na kusababisha msongamano mkubwa kutokana na ukosefu wa barabara mbadala.
“Ikitokea
roli likapata ajali mlima wa Ipogoro na kuziba barabara hali lazima iwe
tete, lakini Serikali imetoa Sh7.75 bilioni kwa ajili ujenzi wa
barabara hii,” alisema.
Moyo alisema shughuli zinazofanyika kwa sasa ni ujenzi wa madaraja na barabara kwa mita 450.
Moyo
alisema fedha nyingine zimetumika kwenye kuboresha miradi ya elimu,
afya, ujenzi wa uwanja wa ndege, machinjio ya kisasa, sekta ya umeme na
biashara.
Aidha
mkuu wa wilaya ya IringaMohamed Hassan Moyo alisema kuwa katika sekta
ya afya walipata zaidi ya bilioni 5 ambazo zimetumika katika ujenzi
ujenzi wa Hospitali,vituo vya afya na zahanati.
Alisema
kuwa kiasi cha zaidi ya bilioni 2 zilitumika katika sekta ya elimu
msingi kwenye ujenzi wa madarasa,ofisi za walimu,nyumba za walimu na
vyoo wakati zaidi ya kiasi cha bilioni 4 zilitumika katika kuboresha
miundombinu ya majengo ya shule za sekondari ambapo walitumia katika
ujenzi wa madarasa,ofisi za walimu,nyumba za walimu na vyoo.
Moyo
alisema kuwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania samia
Suluhu Hassan ameboresha sekta zote katika wilaya ya Iringa ambapo
ametoa kiasi bilioni 93.1 katika sekta za afya,elimu,maendeleo ya
jamii,maji,umeme,biashara na mapato,usafiri,ujenzi na barabara
Alisema kuwa kwa kiasi kikubwa fedha hizo zimechochea ukuaji wa uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Iringa.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya alisema
kazi zilizofanyika zitasaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwenye mji huo.
“Tunaona
kwa macho kazi zilizofanyika, niipongeze Serikali lakini nikupongeze
mkuu wa wilaya kwa kuzungumza haya mbele ya wazee. Vijana wanaweza
kukimbia lakini wazee wanaijua njia, tuwasikilize,” alisema.
Kazi
kubwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiifanya ndani na mwaka mmoja
amefanya mambo mengi Sana na akija Iringa tutampongeza tena-Said Rubeya
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini
No comments:
Post a Comment