Na Baraka Messa, Songwe.
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na afya Taifa (TUGHE) wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kuwaboreshea maslah na kuwafuta machozi wafanyakazi katika utumishi wa umma.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho Joel Kaminyoge katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika katika wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.
Alisema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwafuta machozi wafanyakazi kwa kukubali kuwaongezea mshahara wafanyakazi ahadi ambayo aliitoa siku ya Mei Mosi Jijini Dodoma mwaka huu,
"Japo hakuongea moja kwa moja kwamba ameongeza kwa kiwango gani ,ila tunaimani naye na tunajua jambo letu linnafanyiwa Kazi na taasisi husika" alisema Kaminyoge.
Alisema wao kama wafanyakazi walimuomba Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kiwango cha chini kabisa cha mfanyakazi kiwe shilingi milioni moja na elfu kumi (1,010,000) Ili kukidhi mahitaji kwa wafanyakazi kulingana na namna gharama za maisha zilivyopanda miaka ya hivi karibuni
"Tunashukuru amekisikia kilio chetu na ameahidi kutuongezea japo siyo kwa hicho kiwango tulicho kihitaji tunayo sababu ya kusema asante Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" aliongeza Kaminyoge.
Alisema ni miaka zaidi ya saba kwa sasa imepita bila kuwepo ongezeko lolote la mshahara kuongezeka, lakini kutokana na tamko la Rais Samia Hassan kuwa wafanyakazi wa Tanzania sasa wataenda kuonyesha nyuso za bashasha.
Aidha amezitaka baadhi ya taasisi kuacha manyanyaso kwa wafanyakazi wake wakiwemo wajawazito kwani wanapitia kipindi kigumu kulea ujauzito .
Amesema kipindi cha ujauzito mwanamke anakuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuumwa kutokana na mabadiliko ya mwili inayosababishwa na kiumbe kilichopo Tumboni.
"Kuna baadhi ya taasisi hasa za binafsi huwanyanyasa wanawake na kuwakata mishahara kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa madai kuwa ufanisi wa kazi hupungua sana kipindi hicho cha ujauzito , jambo ambalo ni unyanyasaji mkubwa wa kijinsia" alimalzia Kaminyoge.
No comments:
Post a Comment