ANGALIA LIVE NEWS
Monday, May 9, 2022
DKT.JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE MSOGA
RAIS Mstaafu wa awamu ya Nne,Jakaya Kikwete amehimiza Watanzania kushirikiana na Serikali pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuiendeleza nchi yetu.
Aliyasema hayo ,kama mwananchi wa kawaida kwenye mradi wa kikundi cha vijana Msoga , ambao Mwenge wa Uhuru ulipita kuona shughuli za usafirishaji abiria -pikipiki ambao umegharimu milioni 41.8 kati ya fedha hiyo mil.32.6 Ni mkopo wa asilimia 4 ya vijana kutoka Halmashauri na milioni 9.2 Ni fedha ya wanakikundi .
Kikwete alisema Serikali inahitaji mshikamano wa pamoja na kumuunga mkono Rais, Waziri Mkuu na Serikali ili kufikia malengo kimaendeleo na kiuchumi.
“Hii si shughuli yangu ,nimekuja kushiriki Kama mkazi wa Msoga ,Sina maneno mengi ,naomba tu tushirikiane na Serikali kwa maendeleo yetu wenyewe”alisisitiza Kikwete.
Aliomba viongozi na watendaji kufanyia kazi maelekezo yanayotolewa na wakimbiza mwenge Kitaifa.
Nae mke wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete alisema vijana ndio Taifa la kesho hivyo wajiunge vikundi na kuchapa kazi ili kujiinua kimaendeleo.
Aliwaambia dawa ya kukopa Ni kulipa
“Nawapongeza wakimbiza mwenge ,mnafanya kazi kubwa Sana ,napenda kuwaambia hawana mchezo katika kazi ,Ila Chalinze tumejipanga kwani tunaamini miradi yetu ipo vizuri”
“Hapa ndio Kwetu Msoga, mume wangu ndio kwake, na mwanetu Ni Mbunge wa Jimbo Ridhiwani na tumejiandaa ,tunawakaribisha Sana ,”alisema Salma.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahir Geraruma, alizitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha za vijana , wanawake na wenye ulemavu ili kuimarisha uchumi wa makundi hayo.
Alitoa Rai fedha hizo hizo ziende kwenye makundi hayo Kama Serikali inavyosisitiza kwa manufaa ya vijana ambao wanalia kukosa ajira Lakini wapo wenye moyo wa kujiajiri.
Aliwaasa vijana kuacha kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya na kukipongeza kikundi hicho kwa kuungana .
Awali Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alisema mwenge wa Uhuru ukiwa Chalinze utatembelea miradi 14 yenye thamani ya milioni 937.8 .
Miradi iliyopitiwa ni pamoja a kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto pamoja na upasuaji kwa fedha ya tozo.
Miradi mingine Ni kuzindua mradi wa ukarabati wa barabara Pingo, kufungua vyumba viwili vya Madarasa na ugawaji wa vifaa vya ujenzi vinavyotokana na asilimia 5 ya mchango ya mwenge, kufungua kituo cha afya Sekondari Imperial, mradi wa kisima Kibiki na kuzindua ujenzi wa madarasa manne ya uviko19.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment