Na Said Mwishehe, Michuzi Tv
SHIRIKA
la Childbirth Survival International (CSI) ambalo limejikita kwenye
kampeni ya kuzuia vifo vya mama mjazito na watoto wenye umri chini ya
miaka mitano limeamua kuja na program maalum ya michezo wa mpira kwa
watoto wa kike iliyopewa jina la Masala Princess Girls.
Akizungumza
katika mahoajiano maalum Meneja Programu Vijana kutoka CSI Ester Mpanda
amesema pamoja na kujikita katika kupunguza vifo vya watoto lakini
wamekuwa wakijihusisha na program za watoto wa kike.
“Katika
CSI tuna program tofauti tofauti lakini main program ambayo tunayo ni
Girls Talk, Girls Power ambayo inamhumsisha mtoto wa kike katika makuaji
na maendeleo yake ya kiafya , kimwili na kiakili, CSI ilipoanzisha
program hii ilikutana na wadau mbalimbali na mmoja wa wadau wa muda
mrefu ni JK Youth Pack ambaye amekuwa mdhamini.
“Tumekuwa
tukiita watoto kutoka shule mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam na
kukutana hapa uwanjani kwasababu tunajua ni sehemu ambayo watoto
wanapenda kuja kushiriki michezo, kwa hiyo tunakutana nao na kuzungumza
masuala yanayohusu makuaji.
“Katika
program hiyo mwaka huu tukapata wazo tofauti kidogo hivyo tukaamua
kuanzisha timu ya watoto wa kike ya mpira inayoitwa Masala Princess.
Katika timu ya Masala Princes mimi ni Mtendaji Mkuu wa timu hiyo yaani
CEO na ndio mwanzilishi lakini tunao wakurugenzi, tunao makocha na timu
inafanya vizuri,”amesema Mpanda.
Ameongeza
kutokana na mahusiano mazuri kati yao na JK Pack ambao ni wadhamini wao
wamepewa nafasi ya kufanya mazoezi.Pia wanaye mdhamini mwingine Abec
Company inayojihusisha na vifaa vya ujenzi lakini kwenye Masala Princess
wamekuwa wakitoa vifaa vya michezo.
Akifafanua
zaidi kuhusu Masala Princess, Mpanda anasema katika miaka minne ijayo
wanatarajia kuwa na timu za watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 14 hadi
miaka 17.
“Nia
yetu ni kukuza michezo kwa watoto wa kike, kuimarisha afya na akili,
mtoto akicheza na akili inachangamka.Michezo pia inamuondoa mtoto wa
kike kwenye mambo yanayoweza kuua ndoto zao kama kujihusisha na dawa za
kulevya na mimba za utotoni,”amesema.
Ameongeza kwa hiyo michezo kwao imekuwa na
namba
moja na katika programu ambazo CSI wamefanya Massala Princess ni
miongoni mwa program bora kabisa.“Wakati tunaanzisha program hii
walikuja baadhi ya wasichana wakiwa na changamoto nyingi hata kwa
muonekano.
“Baada
kuanza kujihusisha na program hii ya Masala Princess wameanza
kubadilika. Niwaombe wadau wa mpira hasa wanaojihusisha na watoto wa
kike wasaidie kwani watoto wa kike wanapita kwenye changamoto nyingi
ambazo nyingine ni za kimaumbile.
“
Masala Princess bado ndogo kwa hiyo tunahitaji wadau wengi ili kutimiza
ndoto za wasichana,” amesema na kuongeza watoto wa kike walioko Masala
Princess wanapaswa kupewa tumaini na kuaminishwa kuna maisha mbele yao
na kokote watakakokwenda basi waende kwa ajili ya kuiwakilisha nchi na
wala sio wao au familia zao
No comments:
Post a Comment