Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya ununuzi wa Umma kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho yaliyofanyika katika viwanja vya AICC jijini Arusha.
Maonesho hayo ni sehemu ya wiki hiyo ya manunuzi yenye kauli mbiu ya ‘Matumizi ya teknolojia katika kubiresha ununuzi wa umma’ ilizinduliwa Alhamisi tarehe 5 Mei 2022 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa (Mb) jijini Arusha.
Afisa mtoa taarifa za Usafiri wa Anga Mwandamizi kituo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Bw. Paul Mrema akitoa maelezo ya namna ndege inavyopatiwa taarifa muhimu kabla ya kuanza safari kwa mwananchi aliyefika kwenye banda la TCAA ambapo Mamlaka inashiriki wiki ya ununuzi wa umma inayoadhimishwa Arusha katika ukumbi wa AICC (wakwanza kulia) ni Afisa Muongozaji ndege wa TCAA kituo cha Uwanja wa ndege wa Arusha Bw. Mgaza Emmanuel.
Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akitoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha waliofika kwenye banda la maonesho ya TCAAambapo Mamlaka inashiriki wiki ya ununuzi wa umma inayoadhimishwa Arusha katika ukumbi wa AICC.
No comments:
Post a Comment