ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 18, 2022

CWT KILOLO SERIKALI JENGENI NYUMBA ZA WALIMU

katibu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo (CWT) wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru akiongea mbele ya walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho wilaya ya Kilolo
Mwenyekiti wa chama cha waalimu wilaya ya Kilolo Mwl Mtemi Mgalula akiongea na walimu mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya kilolo akileleza changamoto ambazo walimu wanakutana nazo
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Iringa, Stanslaus Mhongole akiongea na walimu viongozi wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa namna ya kutatua changamoto zao

Na Fredy Mgunnda, Iringa.

Chama Cha walimu ya Wilaya ya Kilolo kimeiomba Serikali ya jamhuri ya muungano was Tanzania kuwajengea nyumba walimu kwenye maeneo ambayo wanafanyia Kazi Ili kuongeza weledi wa Kazi kazini.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa walimu Wilaya ya Kilolo, katibu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo (CWT) wilaya ya Kilolo Anthony Mang’waru alisema kuwa walimu wa Wilaya ya Kilolo Kwa asilimia kubwa hawana nyumba za kuishi hivyo kupunguza hali ya utendaji wa Kazi Kwa walimu.

Mang'waru alisema kuwa serikali imekuwa inafanya Kazi kubwa katika ujenzi ya vyumba vya madarasa na vyoo vya shule lakini imekuwa ikisahau kujenga nyumba za walimu Kwa ajili ya kuishi katika maeneo ya kazi Hali inayowalazimu waalimu wengi kuishi meneo ya mbali na shule kutokana na kukosekana Kwa nyumba za waalimu.

Alisema kuwa walimu wanafanya kazi Kwenye mazingira magumu kutokana na kukosekana Kwa miundombinu ya nyumba za walimu kunakosababisha walimu kushuka Kwa molali ya walimu kufundisha

Mang'waru alisema kuwa baadhi ya shule ukabiliwa na magumu ikiwemo ukosefu wa vyoo kwa ajili ya waalimu hali inayowalazibu kubisha hodi katika makazi ya wananchi walio jirani na shule ambazo walimu hao wanafundisha

kwa uapande wake Mwenyekiti wa chama cha waalimu wilaya ya Kilolo Mwl Mtemi Mgalula alisema kuwa walimuwa wanakumbana na hali ya kustaajabisha, anasema hali ya miundombinu siyo ya kuridhisha kwani pamoja na kuwapo kwa miundombinu chakavu zipo shule zisizo na madara na hata ofisi za waalimu hivyo wanafunzi ulazimika kusomea chini ya mti kama ilivyo kwa waalimu kutumia miti ilipo katika shule zao kuwa ofisi

Kiongozi huyo wa chama cha waalimu wilaya ya Kilolo Mwl Mtemi Mgalula Alisema kuwa shule hizo zimegeuka adhabu kwa waalimu hali inayofifisha morali wa ufanyaji wa kazi ya kufundisha huku akiiomba Serikali kuzipatia ufumbuzi

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo ndiyo alikuwa Mgeni rasmi katika mkutano huu mkuu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo anasema tayari jitihada za utatuzi wa changamoto hizo zinaendelea kwa kutumia nguvu za wananchi pamoja na wafadhiri katika baadhi ya maeneo

Hata hivyo amewahimiza waalimu kuwa wavumilivu wakati serikali inashughulikia changamoto hio huku akiwata wananchi wa kilolo kushirikiana na serikali katika katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya shule ili kuwawezwesha wanafunzi kuwa katika mazingira salama ya kujifunzia

No comments: