ANGALIA LIVE NEWS
Thursday, July 27, 2023
TCAA YATOA UFAFANUZI KUHUSU ZOEZI LA UTAFUTAJI NA UOKOAJI WA NDEGE MKURANGA
Friday, July 21, 2023
Tuesday, July 18, 2023
RAIS SAMIA AMPOKEA RAIS WA HUNGARY, IKULU DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Hungary Mhe. Katalin Novák wakati wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.

RAIS WA HUNGRAY MH. KATALIN NOVAK AWASILI TANZANIA






MKUTANO WA 25 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA SADC KWA NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAANZA JIJINI WINDHOEK
Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) utafanyika jijini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 21 Julai, 2023
Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika tarehe 17 na 18 Julai 2023 ambapo ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati hii unaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Faraji Mnyepe.
Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Balozi Penda Naanda amewakaribisha Wajumbe nchini Namibia na kuwaomba kujadili agenda zilizopo mezani kwa umakini ili hatimaye kuziwasilisha kwa Kamati ya Mawaziri kwa hatua zinazofuata.
Ameongeza kusema kuwa, vikao vya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni muhimu kwani huzikutanisha nchi wanachama kwa ajili ya kujadili na kutathmini hali ya siasa, ulinzi na usalama ya kanda, demokrasia na utawala bora kwa maslahi mapana ya nchi wanachama.
“Nawakaribisha jijini Windhoek na katika kikao chetu hiki ili kwa pamoja tupokee na kujadili taarifa mbalimbali za vikao vilivyotangulia ili kutathimini hatua zilizofikiwa na kutoa mapendekezo yetu ya namna ya kuendeleza mtangamano wa Jumuiya yetu kupitia vikao hivi” alisema Balozi Naanda.
Akichangia hoja wakati wa Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema ni matarajio ya Tanzania kuwa, vikao hivyo ambavyo hufanyika kila mwaka vitaendelea kutoa mchango chanya katika kukuza na kuimarisha masuala mbalimbali ya Jumuiya ikiwemo demokrasia katika Kanda; hali ya Siasa, ulinzi na usalama; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha, ametoa rai kwa Jumuiya ya SADC kuendelea kutilia maanani changamoto ya ongezeko la vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu na wimbi la utekaji nyara Watoto kwa kuwa ni changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri vijana ambao ndio nguvu kazi ya Kanda.
“Ni vyema Kanda yetu ikaendelea kujiwekea mikakati madhubuti ya kudhibiti changamoto hizi ikiwemo kutafuta fedha za kuwasafirisha wahamiaji haramu wanapomaliza vifungo vyao, manunuzi ya magari na vifaa kwa ajili ya kufanyia doria za pamoja za udhibiti wa mipaka na utoaji wa mafunzo kwa taasisi husika” alisisitiza Balozi Fatma.
Kuhusu athari zitokanazo na migogoro ya ndani na nje ya Afrika ikiwemo mgogoro wa Urusi na Ukraine ambao umeathiri usalama wa chakula, Balozi Fatma ameziomba nchi wanachama kuchukua hatua mbalimbali za kujitegemea kwa kuhakikisha zinazalisha chakula cha kutosha, kuimarisha mifumo ya ubora wa mazao, kuwa na soko la Kanda la kuuziana mazao na kuuza nje ya nchi kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.
Mkutano wa 25 unalenga pamoja na mambo mengine kupokea na kujadili agenda mbalimbali zikiwemo mapitio ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 24 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya kanda; masuala ya demokrasia; mapambano dhidi ya uhalifu wa kupangwa, rushwa na usafirishaji haramu wa binadamu.
Friday, July 14, 2023
FANYA HAYA KABLA YA KUSEMA "MWANANMME HATA UMPE NINI HARIDHIKI"

Kama mada inavyojieleza hapo juu, leo tunajifunza kuhusu tabia. Tutaangalia hulka au tabia kwa upande wa wanaume na wanawake. Kizazi cha sasa, kuna desturi imejengeka kwa wanaume na wanawake. Mwanaume anaoa, lakini nje anakuwa na wanawake wengine.
Mwanaume anaweza kuwa ana mchumba ambaye amempa nafasi kubwa ya kuja kuwa mke lakini pembeni anakuwa na mabinti wengine. Hao mabinti anasema ni wa kuzugia. Anawaeleza kabisa kwamba ana mchumba.
Wale mabinti nao wanakubaliana na hali hiyo. Wanakubali kuwa viburudisho wa muda. Wanajua wenyewe wanachokipata. Yawezekana ikawa ni fedha au tu kuridhishwa kimapenzi. Wanawake hao huwa wanakuwa na mbwembwe kwelikweli.
Wanakaba kuhakikisha wanapata wanachokitaka. Matokeo yake humsababishia mwanaume apoteze uelekeo kwa mchumba au mkewe. Kinachotokea huwa ni ugomvi. Wanaharibu uchumba au ndoa za watu.
Hali hiyo ndiyo inayoleta misemo ya wanawake wengi; kwamba mwanaume hata umpe nini haridhiki, wasimuone mrembo barabarani watamtamani.
MATOKEO KIDATO CHA SITA YAPO HAPA
Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed akitangaza matokeo hayo leo.BALAZA la Mitihani Tanzania (Necta) imetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 huku yakionyesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.
Akitangaza matokeo hayo leo Julai 12, 2023 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa ni 47, 340 na wavulana 59, 543.
“Jumla ya watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2023 wamefaulu,” amesema.
Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.
Mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2023.
WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA TAASISI YA UONGOZI KUTOA TAFITI ZA KIMKAKATI



RAIS SAMIA ATOA ARDHI YA HEKARI TANO KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI YA UMOJA WA KUDHIBITI MASWALA YA NISHATI AFRIKA MASHARIKI .


Julieth Laizer,Arusha.
Arusha .Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan ametoa ardhi ya hekari tano kwa ajili ya kujenga ofisi za kudumu ya umoja wa kudhibiti maswala ya nishati Afrika mashariki(EREA )kitakachojengwa mkoani Arusha hivi karibuni.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA ), Dk James Andilile wakati akizungumza katika kikao cha mamlaka ya udhibiti wa nishati kutoka nchi tano za Afrika Mashariki ambazo ni
Uganda ,Rwanda ,Burundi , Kenya na Tanzania.
Dk Andilile amesema kuwa, kituo kitajengwa hapa Arusha na tayari hati zimepatikana na sasa hivi wanaangalia namna ya kuanza utekelezaji haraka ili kuwa na ofisi ya kudumu hapa.
“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutoa ardhi hiyo ambayo itawezesha kujengwa kwa ofisi pamoja na chuo ambacho kitatoa mafunzo kwa wadhibiti wa umoja huo wa Afrika mashariki.”amesema Dk Andilile.
Amesema kuwa ,uwepo wa chuo hicho nchi yetu itanufaika kwani kuna watu watakuja kupata mafunzo hapa na kuna kipato kitaingia kwani watu watapata mafunzo katika chuo hicho na kuwezeshwa uwepo wa ajira kwa wananchi wetu .
Aidha ameongeza kuwa,lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya mambo na kubadilishana mawazo na kufanya mipango kwa ajili ya mwaka wa fedha unaokuja 2023 /24 kuhusiana na shughuli za kiutendaji .
Amesema dhumuni la kuwa na chombo hicho ni kuweka uwiano wa maswala ya udhibiti kisheria kikanuni wa kikanda ili kuchochea uwekezaji katika sekta za nishati ili kuimarisha ustawi wa jamii.
“Umoja wa chombo hicho cha Erea umehusisha nchi tano kutoka ukanda wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni , Uganda ,Rwanda ,Burundi , Kenya na Tanzania na huwa tunakutana mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali .”amesema
.Aidha amesema kuwa,kwa mwaka huu mpaka leo Tanzania ndo ilikuwa ni Mwenyekiti wa chombo hicho cha Erea na katika kipindi hicho ambacho Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wameweza kufanikiwa kukamilisha swala la usajili wa chombo cha Erea na kitaanza kutekeleza majukumu yake kwa kujibu wa sheria.
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza kwenye kikao hicho amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo katika kuhakikisha malengo mbalimbali yanafikiwa kwa wakati na bila kuwepo kwa changamoto zozote.
“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutoa eneo hilo kwani kwetu sisi mkoa wa Arusha kuwepo kwa ofisi hizo hapa kutasaidia sana mkoa wa Arusha kuendelea kukua na kuonekana kuwa kivutio sambamba na kuongeza wimbi la ajira na kukua kwa uchumi na pato la Taifa kwa ujumla.”amesema Mongela
MAANDALIZI YA WORLD CULTURE FESTIVAL 2023 WASHINGTON, DC YAFANYIKA NEWARK, NEW JERSEY
MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI UJERUMANI WAWASILI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA BOMBO
Na Oscar Assenga, Tanga
MADAKTARI Bingwa kutoka nchini Ujerumani wamewasili katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga-Bombo kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa za kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery).
Akizungumza leo mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo,Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Rashid Suleiman alisema kwamba madaktari hao wamekuwa wakishirikiana nao na kwa sasa ni mwaka wa 13 tokea wameanza ushirikianao huo
Wednesday, July 12, 2023
Buku yampa shabiki wa Yanga na Manchester United mamilioni ya M-Bet
Na Mwandishi wetu
Shabiki
wa timu ya Yanga na Manchester United Ezekiel Mwang’onda (34) amesema
ndoto yake ya miaka saba katika kubashiri imekuwa kweli baada ya
kushinda kitita cha Shilingi Milioni 234,272,830 kupitia mchezo wa Perfect12 wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania.
Mwang’onda
ambaye ni mjasiriamali ameshinda mamilioni baada ya kubashiri kwa
usahihi jumla ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.
Alisema kuwa amekuwa akibashiri kwa kipindi kirefu bila mafanikio, lakini mara baada ya kujishughulisha na kampuni ya M-Bet, amepata bahati kwa muda mfupi sana.
“Nimekuwa nikibashiri kwa takribani miaka saba sasa, hivi karibuni, nikaamua kubashiri na M-Bet
kwa sababu kubwa tatu, sababu ya kwanza ni dau, ambapo unatumia sh1,000
tu kubashiri mechi 12, sababu ya pili idadi ya washindi ambao wamekuwa
wakishinda mara kwa mara na tatu, uharaka wa kupata fedha za ushindi na
huduma bora kwa washindi.
Sababu hizi tatu zimenifanya kuhamia huku na sasa nimeingia nyumba ya mabingwa ambao pia ni mamilionea,” alisema Mwang’onda.
Alisema kuwa pamoja na shughuli nyingi kusimama, M-Bet iliendelea kuweka mikeka ya kubashiri ikishirikisha mechi mbalimbali pamoja nanchi za Amerika ya Kusini.
“Mimi
mara nyingi huwa sifuatilii ligi za Amerika ya Kusini, hata hivyo
sikuacha kubashiri na kuendelea kufuatilia kuweka dau na M-Bet
na kushinda kiasi kikubwa cha fedha. Nina majukumu kibao, fedha hizi
nilizoshinda, zitasaidia kukuza biashara yangu na kuwekeza katika miradi
mingine,” alisema Mwang’onda ambaye ni mkazi wa Kyela, mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema Mwang’onda ameungana na washindi wengine wa droo ya Perfect12
na kuwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri
kupitia michezo yao mbalimbali ili kushinda fedha na kubadili maisha.
“Nampongeza Mwang’onda kwa ushindi huu mkubwa na kikubwa zaidi. Nawaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na M-Bet ili kujaribu bahati yao,” alisema Mushi.
BIRTHDAY YA LYSA ILIVYODAMSHI, BIBA APATA MSHANGAO WA SURPRISE
MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI MKUTANO WA SADC TROIKA



RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA JAMII YA WAHADZABE












