Advertisements

Monday, April 15, 2024

DC SAME AMEWATAKA WANANCHI KUHAKIKISHA WANAITUNZA MIRADI AMBAYO IMEZINDULIWA NA MBIO MWENGE 2024


Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe. Kasilda Mgeni (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru, Kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Abdallah Mwaipaya wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, zilipoingia wilayani kwake.


NA ASHRACK MIRAJI, SAME
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe. Kasilda Mgeni, amewataka wananchi kuhakikisha kila mmoja kwenye eneo lake anashiriki kikamirifu kuilinda na kuitunza miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024.

Ameyasema hayo wakati anapokea Mwenge wa Uhuru Wilayani, ambapo miradi kadhaa ya maendeleo imezinduliwa.

Amesema kwa kufanya hivyomiradi hiyo itaendelea kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo kama ilivyokusudiwa katika utekelezaji wake.

Katika Wilaya ya Same, Mmbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zimezindua miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.6.
“Miradi hii ni katika sekta ya barabara, elimu, afya, maji, mazingira, vijana na makundi maalum, fedha ambazo zimetokana na michango ya wananchi, Halmashauri na Serikali kuu.” Alifafanua DC Mgeni na kuonegza. “Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake, sisi Wilaya ya Same tumepokea fedha za maendeleo zaidi ya bilioni 54 ambazo zimetumika katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwemo iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024,” alibainisha.

Alisema ni jukumu letu sasa wana Same kuhakikisha tunailinda na kuitunza miradi hiyo ili iendelee kuwa na manufaa kwa vizazi vyetu vya sasa lakini na vijavyo pia kama ilivyokusudiwa katika utekelezaji wake.


Aidha Mhe. Mgeni, amewashukuru wananchi wa Same lakini pia vijana wa hamasa ya Mwenge kwa kuitikia wito kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamirifu kupokea, kukimbiza pia kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.

“Mmeonyesha uzalendo wa hali ya juu, Serikali inatambua sana mchango wenu vijana kwenye ujenzi wa Taifa, sasa ni wakati wenu kujikita kwenye shughuli za uzalishaji ili muweze kujitegemea kwani Serikali inaendelea kutengenenza fursa nyingi za Maendeleo kwa vijana.” Alisisitiza Mhe. Mgeni.

Pia amesema Serikali ya Wilaya ya Same, imepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi wa Mbio hizo, Godfrey Mzava, ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira kwa kuendele kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali, kuungana kwa pamoja kupinga rushwa, kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa, lakini pia kuacha kuendeleza kilimo cha madawa ya kulevya kwani madhara yake ni makubwa.

No comments: