Wednesday, August 14, 2024

NAIBU WAZIRI LONDO AMTEMBELEA KATIBU MKUU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica Nduva alipomtembelea Ofisini kwake tarehe 13 Agosti 2024 jijini Arusha.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica Nduva alipomtembelea kwa lengo la kujitambulisha tarehe 13 Agosti 2024 jijini Arusha.
mazungumzo yakiendelea.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) katika picha na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica Nduva alipomtembelea Ofisini kwake tarehe 13 Agosti 2024 jijini Arusha.

NAIBU Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) ametembelea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica Nduva Ofisini kwake tarehe 13 Agosti 2024 jijini Arusha.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Londo alimuhakikishia Mhe. Nduva ushirikiano na kumuelezea kuwa Tanzania itashiriki katika masuala yote yanayohusu Jumuiya ya EAC kwa uzito unaostahili.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana baada ya Mhe. Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mwezi Julai 2024.

Mhe. Londo aliongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.

No comments: