Sunday, August 25, 2024

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MSIBA WA MKE WA MNADHIMU MKUU WA JWTZ


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Agosti 24, 2024 amehani msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi.
Akizungumza kwa Niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo.
“Rais Dkt. Samia anatoa rai kwa waombolezaji wote kuendelea kuiombea familia hii katika kipindi hiki cha huzuni”.


No comments: