ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 30, 2024

MUHIMU KUENDELEZA JITIHADA ZA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI ILI WAWEZE KUZITUMIA IPASAVYO FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA UTALII



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la ufunguzi wa Mradi wa Utalii Rafiki na Mazingira katika Msitu wa Masingini Wilaya ya Magharib "A" Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukifu ya Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanziar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ni muhimu kuendeleza jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi ili waweze kuzitumia ipasavyo fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Msitu wa Masingini Wilaya ya Magharib "A" Unguja alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa Utalii Rafiki na Mazingira, unaomilikiwa na Kampuni ya Zanzi Eco- Tourism wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia tisa ikiwa ni shamra shamra za kuelea maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amefahamisha kwamba Zanzibar kupitia rasilimali za asili kama vile misitu upo uwezekano mkubwa wa wananchi kuwekeza na kuweza kupata faida na kwamba kampuni iliyoanza kuwekeza kwenye msitu wa masingini imeonesha njia.
Hivyo Mhe. Othman amesisitiza kwamba suala la hifadhi ya mazingira ni muhimu kwa maisha ya wanadamu na kwamba Kampuni hiyo ni vyema kupanua wigo wake na kuwekeza sehemu nyengine katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Amezitaka wizara za kilimo na Mamalaka zinazohusika na uwekezaji kutafuta wawekezaji wengine zaidi kuwekeza katika miradi rafiki na mazingira kwenye misitu tofauti ya hifadhi iliyopo katika visiwa vya Unuja na Pemba kwani kufanya hivyo kutaweza kuleta tija zaidi kiuchumi kupitia maliasili hiyo .
Hata hivyo, Mhe. Othman amesitiza haja ya Mamlaka zinazousika na hifadhi ya Misitu kuendelea kuilinda msitu huo wa Masingini kwa kuwa ni chanzo kikubwa cha upatikanaji wa Maji katika maeneo mbali mbali ukiwemo mji wa Zanzibar na pia upatikanaji wa hewa safi na salama kwa uhai wa wanadamu.

Hatua hiyo amesema itasaidia katika kuhakikisha misitu na rasilimali zake inakuwa endelevu na kwamba ni muhimu kwa wananci kujenga tabia ya kulinda na kihifadhi misitu ili matunda yake yaendelee kunufaisha sasa na vizazi vijavyo.
Amesema kwamba Zanzibar ikilelea na uwekezaji wa miradi ya aina hii ni wazi kwamba itachangia sana kutatua changamoto za kimazingira ikiwemo uvamizi holela wa Misitu pamoja na ukataji wa miti.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo , Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema kwamba mradi huo awamu ya kwanza utasaidia kukamili changamoto ya uharibifu wa Mazingira kwa kurejesha shukrani kwa wananchi kwa kuwapa gaiwio la faida linalotokana na uwekezaji huo.
Aidha amesema pia mradi huo unaibua fursa zaidi ya kuongeza vivutio vya na fursa zaidi za utalii ili kufikia matumaini ya taifa katika suala la kukuza ajira kwa wananchi.

Naye mmiliki wa Mradi huo Alan Peter Nnko, amesema kwamba mbali na hifadhi ya mazingira mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa wanawake kusaidia ajira na kueleza kwamba awamu ya kwanza ya maradi huo, utakaokuwa na daraja la kuangalia msitu, mkahawa, nyumba ya juu ya miti , daraja la kunesanesa na vivutio vyengine na hadi sasa ushagharimu zaidi ya shilingi milioni mia tisa.

Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo Jumapili Disemba 28 mwaka 2024.














No comments: