Mafunzo ya usimamizi wa mapato na utoaji huduma bora yanafanyika kuanzia tarehe 1/6/2026 hadi 4/6/2026 katika Hifadhi ya Taifa Tarangire .
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara TANAPA,Kanda ya Kaskazini na Hifadhi ya Taifa Tarangire yamejumuisha washiriki kutoka Hifadhi tano (5)ambazo ni Tarangire,Ziwa Manyara ,Arusha , Mkomazi na Kilimanjaro.
Akifungua Mafunzo hayo Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tarangire ,Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dr Tutindaga George alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa watumishi katika kusimamia ukusanyaji wa mapato , kutoa huduma bora na kusimamia shughuli za utalii hasa tunapoelekea msimu mkubwa wa utalii.
Kupitia mafunzo hayo washiriki wamejifunza mbinu mbalimbali za uthibiti wa mapato pamoja na kufanya ukaguzi katika hoteli na kambi za kitalii pamoja na kujifunza usimamizi wa shughuli za utalii ndani ya Hifadhi.
Hatua hizi zinaendelea kuimarisha uwajibikaji , ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ,huduma bora na uhifadhi endelevu wa rasilimali za utalii nchini.
Mafunzo haya yataendelea kwa Hifadhi zingine zilizopo Magharibi, Mashariki na Kusini mwa nchi ili kuweza kujipanga na kuweka mikakati thabiti katika utoaji wa huduma za utalii.








No comments:
Post a Comment