ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 6, 2026

UONI HAFIFU WAONGOZA CHANGAMOTO KWA WANAOPIMA MACHO BANDA LA MUHIMBILI NANE NANE



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema tatizo la uoni hafifu linaongoza miongoni mwa changamoto zinazobainika kwa wananchi wanaofika kupima afya ya macho katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Dk. Samweli Malechela, jijini Dodoma, ambapo huduma za uchunguzi wa macho, elimu na ushauri wa kitaalamu zinatolewa bure. 

Akizungumza Dkt. Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Johannes Mafwili, amesema wananchi wengi wanaofika katika banda la hospitali hiyo hupatikana na tatizo la uoni hafifu, huku wakifanyiwa uchunguzi wa kina na kupatiwa ushauri wa kitaalamu kulingana na hali zao. 

Amesema uchunguzi wa mapema husaidia kubaini magonjwa mbalimbali ya macho kabla hayajasababisha madhara makubwa, hivyo amewahimiza wananchi kutumia fursa ya maonesho hayo kupima afya ya macho bila kusubiri dalili kuwa mbaya. 

Dkt. Mafwili amewataka wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nane Nane kufika katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kunufaika na huduma hizo za bure na kupata elimu itakayowasaidia kulinda afya zao.











No comments: