Saturday, February 13, 2010

Anayetumia jina langu kutafuta ubunge hafai

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wananchi wasiwasikilize wanaojipitisha kujitangaza kuwania ubunge na udiwani katika majimbo nchini wakitumia jina lake kwa sababu hajawatuma.

Amelipongeza Bunge kwa kazi nzuri katika kipindi chote cha miaka mitano tangu aingie madarakani, kwa kuwawakilisha vyema wananchi ikiwa ni pamoja na kupitisha miswada muhimu kwa Taifa, ukiwamo wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2009 uliopitishwa na Bunge hilo juzi.

Ameyasema hayo katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya na kuipongeza Klabu ya Michezo ya Bunge, iliyofanyika juzi usiku katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. 

No comments: