Tuesday, October 22, 2024

DKT. MWAMBA AJADILI UFADHILI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akijadili kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Katikati ni mwongoza majadiliano (Moderator) ambaye ni Waziri wa Fedha wa Uganda, Dkt. Ramathan Ggoobi, na kulia ni Mtoa Mada, Bw. Reginald Max, ambaye ni Mshauri Mwandamizi wa masuala ya Miundombinu na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB).
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akijadili kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati), akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Uganda, Dkt. Ramathan Ggoobi (kulia), na Mshauri Mwandamizi wa masuala ya Miundombinu na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB), Bw. Reginald Max, baada ya kushiriki mjadala (Panelists) kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Mawaziri wa Fedha, Makatibu Wakuu na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), maadhimisho yaliyoambatana na mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakiwa katika picha na Waziri wa Fedha na Maendeleo wa Lesotho, Dkt. Retselisitsoe Adelaide Matlanyane (Mb), katika hafla ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), maadhimisho yaliyoambatana na mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
(Pich ana Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha, Washington D.C, Marekani)

Na Benny Mwaipaja, Washington D.C, Marekani
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ametoa wito kwa Benki Kuu za Nchi za Afrika, kuweka mipango na mikakati ya kutafuta fedha kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kwa ajili ya kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabianchi katika nchi hizo.

Dkt. Mwamba ametoa rai hiyo wakati akishiriki mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Alisema kuwa mbinu mahususi ikiwemo uanzishwaji wa hati fungani za kijani zenye lengo la kuvutia uwekezaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kusimamia ipasavyo Taasisi za fedha kuwekeza kwenye kilimo kwa kutoa mikopo, zitasaidia kukuza uchumi wa nchi hizo za Afrika na maendeleo ya watu wake.

Dkt. Mwamba alibainisha katikaTukio hilo lililowakutanisha Mawaziri wa Fedha, Makatibu Wakuu na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika, kwamba mabadiliko ya tabianchi yameziathiri nchi nyingi ikiwemo Tanzania na kwamba upatikanaji wa fedha kwa njia shirikishi katika kukabiliana na athari hizo kutaimarisha uchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MEFMI, Dkt. Louis Kasekende, alisema kuwa Taasisi yake imejipanga kuwawezesha wanachama wake kuweka mipango ya pamoja ya kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na usimamizi wa uhimilivu wa madeni ya nchi za Afrika.

Mbali na Dkt. Mwamba, washiriki wengine katika mkutano huo kutoka Tanzania, walikuwa Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Sera za Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

No comments: