Saturday, February 13, 2010

Serikali Ivory Coast yavunjwa


Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ameivunja serikali yake pamoja na tume ya uchaguzi, hatua ambayo inazua wasiwasi wa lini uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu utafanyika.
Muda wa kuwa madarakani kwa Rais Gbagbo ulimalizika mwaka uliopita.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Guillaume Soro ameagizwa kuunda serikali mpya.
Bwana Gbagbo ameishutumu tume ya uchaguzi kwa kujaribu kuongeza zaidi ya watu laki nne katika daftari la kudumu la wapiga kura kinyume cha taratibu.
Upinzani unasema kuwa wengi wa watu hao wanatoka katika makabila madogo ambao hayamuungi mkono Bwana Gbagbo.
Katika wiki mbili zilizopita, wafuasi wanaomuunga mkono rais Gbagbo wamekuwa wakijaribu kutumia mahakama kuondoa maelfu ya majina watu kutoka daftari la wapiga kura wakiwashutumu kuwa ni raia wa kigeni.

No comments: