Monday, February 8, 2010

Mechi Yanga na Simba Kuchezwa April 4

Timu ya Stars United
Timu ya Simba
Timu ya Yanga

Mechi ya kwanza ya Simba na Yanga mwaka huu itafanyika jumapili april 4,kwenye uwanja wa Kalmia,hii ni kufuatia mechi itakayochezwa jumamosi kati ya Stars united na Maryland united japo uwanja itakapochezwa mechi hiyo bado kutangazwa.

Mtayarishaji wa mpambano huo wa Stars na Maryland United,Cyprian,amesema kutakua na nyama choma siku hiyo ya jumamosi april 3,na mechi hii ni re-union ya wachezaji wote wa maryland united na kutakuwa na zawadi maalum kwa wachezaji wazamani wa timu hiyo.

Wachezaji Watanzania waliowahi kuichezea Maryland united ni Liberatus Mwang'ombe,Vicent Ndusilo,Chiwa Mwombela,Elvis Dotto na Yahaya Kherina,na Cyprian ameiomba Stars united wachezaji hao wachezee Maryland united siku hiyo ya mpambano.

Salum Salum amesema yeye hana mkwara wowote,wachezaji hao wanaweza kuchezea timu hiyo,lakini wajue hawatakiwi kuifunga timu yao,mchezaji yeyote atakaeifunga timu yake ya Stars united ajue amefungiwa wewe chezea tu lakini ujue unatoa pasi tu,

No comments: