Ikiwa ni siku chache tangu aondoke kuelekea nchini China, mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la Miss World 2010, Genevieve Emmanuel amepiga picha moja ya nusu uchi, Ijumaa limeiona.
Picha hiyo inayomuonesha mrembo huyo akiwa amevalia kichupi chekundu pamoja na sidiria ya maua tu imetundikwa katika mtandao wa Miss World pamoja na maelezo yanayomhusu.
Wakiizungumzia picha hiyo baadhi ya wadau wa mashindano hayo wameendelea kukandia uvaaji huo kwa maelezo kuwa, ni kinyume na utamaduni wa kitanzania.
Walisema kuwa, wanajua miongoni mwa taratibu za shindano hilo ni pamoja na mshiriki kupiga picha za aina hiyo lakini wakaeleza kuwa, inakuwaje picha kama hiyo itakapoonwa na wazazi hasa baba yake.
“Hatushangai sana kuona mrembo kapiga picha kama hii kwani ndivyo wanavyofanya kila mwaka lakini ni aibu na lazima tuendelee kukemea,”alisema Farida wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Naye John wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa, kuna kila sababu ya shindano hilo kuangaliwa upya kwani kwa namna moja linakwenda kinyume na tamaduni za baadhi ya washiriki.
“Juzi kulikuwa na lile shindano la Miss Universe, mwakilishi wetu alitakiwa kupiga picha akiwa na chupi tu akagoma yeye na wenzake, yamefanyika mashindano ya Miss Progress hakuwa na kuvaa vivazi hivyo vya aibu, kwanini Miss World wanaving’ang’ania?” Alihoji msomi huyo.
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS
1 comment:
Jamani kwani baba akiona bintiye amevaa hivyo kuna nini? Mbona alivyokuwa mdogo baba huyo huyo alikuwa anamisha nepi? Sasa kakua hajaonyesha alichopewa na mamaye ameficha kwa japo nguo kidogo sijaona tatizo lake. Kama ni hivyo ni bora TZ ijitoe ktk mashindano kama hayo. Mbona Iran haishiriki kwa sababu inalinda maadili yake kwa nini TZ wasigome kushiriki ikajulikana. Pls, acheni kubwabwaja huko TZ mitaani visichana vinatembea utadhani vililazimishwa kuvaa nguo za wadogo zao.Acheni hizo jamani.
Post a Comment