Rais Jakaya Kikwete akikata keki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwake iliyofanyika Dar es Salaam juzi usiku.Wanaoshuhudia ni mkewe Mama Salma na mjukuu wao Karima. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlisha kipande cha keki mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwake miaka 60 iliyopita.Sherehe hizi zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimlisha kipande cha keki Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe ya kumpongeza Rais Kikwete kwa kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake jana jioni.Sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.,kulia kwake ni Mama Salma Kikwete. Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd,Juhayna Ajmi.Rais Kikwete alipita kila meza kusalimiana na wageni waalikwa waliofikwa kwenye hafla yake fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia leo. Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay pamoja na Mwana FA wakizungumza jambo na Rais Kikwete na pia kumpa pongezi za dhati kabisa kwenye hafla hiyo iliyokuwa ya kuvutia usiku wa kuamkia leo. Mtangazaji mahiri wa Clouds FM,Eprahim Kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Morroco Rais Kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.Timu hiyo itacheza na timu ya Taifa,Taifa Stars hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Picha na Ahmed Michuzi na Freddy Maro/IKULU |
No comments:
Post a Comment