Sunday, January 30, 2011

Nawakaribisha wadau wote Millenium fika tukake keki ya mwaka mmoja wa VIJIMAMBO,bila nyinyi Vijimambo isingefikia hapa ilipo leo,shukrani zangu za dhati kwanza kwa wadau wooote wa Vijimambo,Mh.Blozi Mwanaidi Maajar,maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi,Washington,DC, Kalley Pandukizi,Jojo,Michuzi blog,Haki Ngowi,Bongo Celebrity,Lady Jay Dee Blog,Changamoto yetu,swahili villa,Sunday Shomari Blog,wafanyakazi wa Green Grocer kwa mchango wao wanaonipatia kila siku tukutanapo kazini,na wengine wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika kufanyikisha Blog hii ya VIJIMAMBO isonge mbele 
hii chini ndio idadi ya wadau waliotembelea blog hii tangia 2010 May-2011 January.
United States
182,659
Tanzania
15,868
United Kingdom
6,236
Canada
5,532
Netherlands
1,676
Kenya
594
Germany
583
Sweden
531
Norway
512
France
408

asanteni sana na Mwanyezi  Mungu awazidishie saba mara sabini

KUMBU KUMBU
Habari hii ndio iliyokua ya kwanza hewani siku ya January 31,2010 ilipaishwa (3:37pm) 
Nyama Choma DMV


Kikosi cha Stars united kikiwa Houston

Kutakuwa na NYAMA CHOMA na mechi ya mpira wa miguu kati ya Stars united na Maryland United siku ya jumamosi april 3rd 2010 kiwanja au park itakayofanyikia bado kutangazwa,inasemakana huenda ikafanyikia Greencastle park iliyopo Brigs chaney,Silver Spring.

Mtayarishaji wa mechi hii,Syprian Kumalo amabe ni raia wa Bondeni mwa AFrika,amesema hii mechi ni kuwazawadia wachezaji wa zamani walio wahi kuichezea timu ya Maryland United.

Wachezaji Watanzania waliowahi kuichezaea timu hii ni Vicent Ndusilo,Liberatus Mwang'ombe,Elvis Dotto Mnyamuru na Chiwa Mwombela

Na hii ni habari nyingine iliyopaishwa siku hiyo January 31,2010(6:33pm)
Stars United,Uganda na Zambia kuchuana Boston,April 23

Stars United
Zambia

Uganda

No comments: