Advertisements

Wednesday, January 12, 2011

Zoezi la uchaguzi wa awali wa Rais Nigeria laanza-VOA

Goodluck Jonathan (kushoto) na  Atiku Abubakar
               Goodluck Jonathan (kushoto) na Atiku AbubakarPicha ASSOCIATED PRESS

Chama tawala cha Nigeria kimepitisha wagombea watatu katika uchaguzi wa awali wa Alhamisi.

Rais Goodluck Jonathan atashindana na makamu rais wa zamani Atiku Abubakar na mwanasiasa mkongwe Sarah Jibril kuwa mgombea wa chama cha Peoples Democratic Party.

Baadhi ya watu huko Nigeria wamepinga ugombeaji wa Bw. Jonathan lakini jumatatu mahakama moja ya Nigeria ilitupilia mbali shitaka lililowasilishwa na wanachama watatu wa PDP waliokuwa wakijaribu kumzuia Bw.Jonathan kugombea.

No comments: