Advertisements

Wednesday, January 12, 2011

Ndama Mutoto ya Ng'ombe mbaroni kwa wizi!

Watoto wa Afande Mwema (Jeshi la Polisi) linamshikilia mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani (38) a.k.a Ndama mutoto ya Ng'ombe kwa tuhuma za kukutwa na mkoko (Gari) wa wizi.

Pamoja na Ndama, wengine wanaoadaiwa kuhusika na wizi huo ni Sylvester Mashindila (45), Richard Marimi (46), Peter Goyayi (30) au Makoye wakazi wa Mwananyamala kwa Kopa na Charles Mwita (43) mkazi wa Kinondoni.


Akichonga na waandishi wa habari,Kamanda wa Kanda Maalum Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walipora gari aina ya Hino lenye namba FDIJKD 11185 maeneo ya Tunduma mkoani Mbeya.

Kova alisema kikosi Maalum cha Kupambana na Wizi wa Magari ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam kilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wanaodaiwa kumnywesha dawa za kulevya aliyekuwa dereva wa gari hilo kabla ya kumpora.

Alisema gari hilo lilibeba bidhaa mbalimbali vikiwemo vitanda vinne, magodoro, majokofu, makochi na majiko ya umeme ambapo watuhumiwa hao baada ya kutenda tukio hilo walikimbilia mafichoni jijini Dar es Salaam na kuvihifadhi vitu hivyo Mbezi nyumbani kwa Ndama.

                                        chanzo:darhotwire

No comments: