ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 3, 2011

15 wakamatwa Sudan wakipinga bei kupanda-BBC

Takriban waandamanaji 15 wamekamatwa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum katika kile ambacho wanaharakati wanasema ni maandamano ya kupinga kupanda bei za bidhaa katika miji mingine.
Maandamano Sudan
Maandamano Sudan
Zaidi ya watu 100 wametiwa mbaroni hadi sasa tangu kuanza maandamano hayo siku ya Jumapili, kwa mujibu wa kikundi kinachotetea haki za binaadamu, Africa Centre for Justice and Peace Studies .

Polisi wanakanusha taarifa kwamba mwanafunzi mmoja aliuwawa katika maandamano mapema wiki hii.
Waandishi habari wanasema inaelekea maandamano hayo yametayarishwa kupitia tovuti, yakihamasishwa na matukio ya Tunisia and Misri.

Siku ya Jumanne waandamanaji kadhaa walikusanyika katika uwanja wa Jackson Square, mojawapo ya vituo vikuu vya basi mjini Khartoum, pale vikosi vya usalama vilipowavamia na kuwatia mbaroni watu kadhaa waliokuwepo hapo.
Wakereketwa wanaotetea haki za binaadamu wanasema idadi ya watu waliokamatwa huenda ikafika 30.
Wanahisi huenda ulikua mtego wa vikosi vya usalama ambavyo walivishutumu kwa kuweka ujumbe kwenye mtandao wa Facebook kuwataka watu washiriki katika maandamano.
Mwaandishi wa BBC James Copnall akiwa mjini Khartoum anasema kulikua na maandamano mengine siku ya Jumanne usiku mjini Khartoum na mji pacha wa Omdurman.
Maandamano hayo yametayarishwa zaidi na wanafunzi na yamedhibitiwa zaidi katima maeneo ya vyuo vikuu.

No comments: