Kabla hujapanga kumshawishi mtu aliyekuvutia katika mazingira unayoishi, hakikisha unazijua mbinu kadhaa za kutumia. Ikiwa kama hauko tayari kumkosa anayeutesa moyo wako kimapenzi hakikisha unafuta njia zifuatazo.
-Tabasamu; Tabasamu la mara kwa mara. Hii ni mbinu nyepesi zaidi ya kuushawishi moyo wake. Wavulana wengi hupata urahisi wa kutupia ndoana pale wanapokutana na wasichana waliojaa tabasamu.
-Tabasamu; Tabasamu la mara kwa mara. Hii ni mbinu nyepesi zaidi ya kuushawishi moyo wake. Wavulana wengi hupata urahisi wa kutupia ndoana pale wanapokutana na wasichana waliojaa tabasamu.
-Kuwa jinsi ulivyo; Jikubali kutokana na muonekano wako jinsi ulivyo. Usiwe mtu wa kujivika uhalisia wa watu wengine, ukajifanya na wewe ni kama msichana fulani unayedhani anavutia. Usimwige mtu anavyoongea au anavyotenda, kumbuka wewe ni wewe na yule ni yule.
-Zungumza kidogo, sikiliza zaidi; msichana anayetaka kumvuta mwanaume lazima ahakikishe kuwa nakuwa na tabia ya kupenda kusikiliza zaidi kuliko kusema. Siku hizi wanawake wamekuwa waongeaji mno kiasi cha kuwafanya wanaume wahisi kuwa wakiwa nao watazidiwa maneno na kupoteza utawala.
-Usivae mavazi yanayokuzidi saizi; Hii ni pamoja na mapambo na jinsi unavyo vaa. Mara nyingi vaa mavazi yaliyo ‘simpo’ lakini ya kuvutia na yanayoendana na mwili wako yaliyo katika ‘staili’ za kisasa zaidi. Pendelea kuvaa nguo za saizi ya chini na tembea kwa mwendo wa madaha.
-Kuwa mcheshi; Usiwe mtu wa kununanuna bila sababu. Jitahidi kadiri uwezavyo kuwa mtu mcheshi unayeweza kubadilia jambo baya kuwa zuri. Wanaume wengi hupenda wanawake wacheshi huamini wakiwapata hao watazifanya familia zao kuwa na furaha.
- Tumia Pafyumu Nzuri; Wavulana huweza kumtambua zaidi msichana hasa waliozoeana kwa manukato yake mazuri. Hakikisha wakati wote mwili wako hautoi harufu mbaya.
-Zingatia Usafi; Hakikisha unaonekana nadhifu kila wakati. Ufanye mwili wako kuwa msafi tangu kucha mpaka nywele. Usijipende kuvaa ngua chafu zenye harufu ya jasho na zilizochakaa.
-Usijirahisi sana; Hata kama unataka kumvuta kimapenzi haifai kujipendekeza sana kwake, yaani kujipitisha pitisha na kujigonga kwa maneno. Jiheshimu na uwe makini katika kutunza siri ya kile ulichokusudia kufanya. Usiache watu wa pembeni wajue mapema nia yako.
-Badilika mara kwa mara; Kamwe usimwache mwanaume akufahamu kwa kila kitu. Kosa kubwa linalowagharimu wanawake wengi ni kujiweka wazi mno mapema. Mwanzo tu anaanika mpaka siri za ukoo wake ulivyowahi kusumbuliwa na pengine hata magonjwa yanayomsumbua kila mara.
-Jiamini; Kujiamini humaanisha kutoogopa kuongea jambo lolote la muhimu. Jenga hoja za busara kila mara.
Muangalie machoni zaidi. Usiwe mtu wa aibu kupita kiasa. Wanaume hupenda wanawake wanaojiamini katika maisha yao, wenye uwezo wa kukabili changamoto za maisha na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment