ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 25, 2011

Dereva ajali ya Five Stars akamatwa

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limemtia mbaroni dereva wa gari lilosababisha vifo vya wanamuziki 13 wa kundi la muziki wa taarabu la ‘Five Star’ na wengine 12 kujeruhiwa katika eneo la Doma nje kidogo ya Hifadhi ya Mikumi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Adolphina Chialo, alimtaja dereva huyo kuwa ni Juma Hassani (31), mkazi wa Dar es Salaam na kwamba alikamatwa Juni 21, mwaka huu mchana katika kituo cha Polisi Mikumi wilayani Kilosa.

Chialo alisema dereva huyo anatarajiwa kupelekwa Kilosa ili aweze kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya kujibu tuhuma hizo.
Dereva huyo anadaiwa kusababisha vifo vya wanamuziki 13 na kujeruhi wengine 12 Machi 22, mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku, eneo la Doma katika barabara ya Morogoro - Iringa.
Alilitaja gari lilokuwa likiendeshwa na dereva huyo na kusababisha vifo hivyo kuwa ni lenye namba za usajiri T 351 BGE Toyota Costa, na kwamba lilikuwa ikitokea wilayani Kyela mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
Wanamuziki waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni Issa Kijoti, aliokuwa akitamba na wimbo wa ‘Nichumu,’ Nassoro Madenge, Omary Hashim,Hassan Ngereza, na Husna Mapande.
Wengine ni Hamisa Musa,Tizo Mpunda, Rama Kinyoya, Jumanne Maarufu kasheba, Shebe Juma, Omary Tall, Haji Mzamila, pamoja na wengine waliofahamika kwa jina mojamoja ambao ni Haji na Maimuna.
CHANZO: NIPASHE

No comments: