ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 10, 2011

BONGO REAL YAIFUNGA KWA TAABU UBALOZI 8-3

 Timu ya Bongo Real FC(Chama Kubwa)
Timu ya Ubalozi
Timu ya Bongo Real FC ya DC inayoundwa na wachezaji waliocheza mpira siku nyingi jana katika viwanja vya Meadowbrook park iliichezesha mchakamchaka timu ngumu ya Ubalozi kwa kuibanjua 8-3 mpaka mapunziko Bongo Real ilikua mbele kwa goli 4-0 magoli matatu yaliyofungwa na nyota wa mchezo wa jana Fadhil Londa ambae jana alikua mwiba kwenye timu hiyo ya Ubalozi.

Idd Shah
 Mchezo ulianza kwa timu ya Ubalozi kulishambulia goli la Bongo Real lakini umaliziaji haukua mzuri katika dkk ya 6 ya mchezo,mchezaji wa Ubalozi Rony Maganga alikosa goli la wazi alipokua amebaki yeye na golikipa kwa kupiga shuti lililotoka nje sentimita chache.
Refa Seif Mohamed
Baada ya shambulio hilo Bongo Real ililiandama goli la timu ya Ubalozi kama nyati aliyejeruhiwa na kunako dkk ya 10,Fadhili Londa aliipatia timu ya Bongo Real goli la kuongoza.Na kunako dkk ya 18 Fadhili Londa tena aliweka mpira Kimiani kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Ubalozi,Dany Star.

Kutoka shoto ni Maneno Uvuluge,Mkuu wa Mkoa DC,Saleh Mohammed,Maestro King Kiki na Andy Swebe
Wachezaji wengi wazoefu wa timu ya Ubalozi hawakuwepo jana kutokana na wengi wao kusafiri kikazi inawezekana ndio  chanzo cha timu hii kufungwa goli hizo.

Ni Londa tena anayepata bao la tatu kunako dkk ya 37 kwa shuti la mbali ambalo Dany Star hakujua la kufanya na Rich alifunga ukurasa huu wa kwanza kwa kufunga goli la nne baada ya kutokea piga ni kupige kwenye goli la Ubalozi.
Golikipa Mahili Seif Msabaha
Kipindi cha pili kilianza na kilionyesha uhai kidogo kwa timu ya Ubalozi kwa  kosa kosa walizokua wakionyesha mara kwa mara lakini bahati haikua yao na kupelekea kufungwa goli la tano na mchezji Seif Kadria kwa shuti kali ndani ya kumi na nane.

Kutoka kushoto ni  Seif Mohamed,Alawi Omar,Faraja Isingo naYasin Randy
Baada ya goli hilo timu ya Ubalozi ilionyesha uhai kidogo illipojaribu mashabulizi ya kusutukiza na kujipatia lililofungwa na Abuu Swahili Villa kwa shuti la mbali la kushutukiza

Mapaka dkk 90 Bongo Real 8-3 Ubalozi

No comments: