ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 5, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Basi la abiria la Kampuni ya MK likiwa kando ya barabara ya Morogoro, baada ya dereva kuacha njia na kuliingiza porini wakati akipisha msafara wa Rais Jakaya Kikwete, ulioibuka ghafra, ukielekea Charinze, mkoani Pwani juzi. baadhi ya abiria walipatwa na mshituko.
Balozi wa Afrika ya Kusini, Bw. Henry Chiliza, akiweka shada la maua kwenye moja ya makabuli ya wapigania uhuru wa nchi hiyo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maridhiano na kumbukumbu ya mapambano ya ukombozi Kusini mwa Afrika, yaliyofanyika kwenye kambi ya Dakawa, mkoani Morogoro juzi.
Meneja wa Kitengo cha M-Pesa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Bi. Nabwike Kibona (kushoto) akimuandalia chai Bw. Ramadhani Abdalah ambae ni mtoto yatima anayelelewa katika kituo cha Mwana Orphans Centre cha Vingunguti, Dar es Salaam jana,  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care inayofanyika kila mwisho wa mwaka kuwasaidia mahitaji ya watoto yatima wakati wa sikukuu za krismas na mwaka mpya.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Bw. Paul Chizi (aliyeketi), akiongea na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa sare mpya za wahudumu wa ndege za shirika hilo.
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma za Asili cha Dakawa, wakicheza ngoma ya mapigano  ya Bugobogobo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mariadhiano ya Taifa la Afrika ya Kusini, iliyofanyika kwenye Kambi ya wapigania Uhuru wa nchi hiyo mjini Dakawa, Morogoro mwishoni mwa wiki.(picha zote kwa hisani ya Majira)

No comments: