ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 5, 2012

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Maofisa kutoka Manispaa ya Ilala, Bw. Uswege Abel (kulia), ambaye ni Mthamini wa Majengo na Ofisa Ardhi, Bi. Fatuma Rashid, wakisindikizwa na Polisi jana, kuhakiki nyumba za wakazi wa Jangwani Magharibi, walioathiriwa na mafuriko, yaliyotokea Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya waathirika wa mafuriko, wanaoishi kwenye Kambi iliyoko Shule ya Msingi Gilman Rutihinda, Kigogo, Dar es Salaam wakipata matibabu, kutoka kwa wauguzi wa Manispaa ya Ilala jana, Bi. Frola Chilwa. (kushoto) na Teddy Uledi.
Naibu Katibu Mkuu, Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Julius Mtatilo (kushoto), akikabidhi msaada wa mfuko wa unga wa sembe jana kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigogo, Bw. Emmanuel Riwa, kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu, Uchumi na huduma za Kijamii, Dkt. Bartholomew Bwire Rufunjo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu hatua ya uendelezaji wa sekta ya miundombinu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na Prona Mumwi)
Kiungo wa timu ya soka ya Kimara Kids, Bosingwa Pankras (kulia), akiondosha hatari langoni mwake, huku mshambuliaji, Juma Mohamed wa New Boys ya Gongolamboto, akitaka kumnyang'anya katika mchezo maalumu ulioandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana. (picha kwa hisani ya Majira)

No comments: