Tausi Ally na Nora Damian
CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 48 za kutoa malipo ya madaktari wote mara moja ili waweze kuendelea kufanya kazi ya kuwahudumia Watanzania.Wakati MAT ikitoa onyo hilo, mgomo wa madaktari 229 walio katika mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jana uliendelea huku madaktari hao wakisisitiza kwamba hawatakuwa tayari kurejea kazini hadi hapo watakapolipwa fedha zao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi aliitaka Serikali kuheshimu kazi ya udaktari na huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi na iepuke kuwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara katika sekta ya afya.

“Iwapo wizara itashindwa kushughulikia malipo haya ndani ya saa 48, basi itatulazimu kuitisha mkutano wa dharura kwa madaktari wote nchini ili kutafakari mustakabali wa jambo hili nyeti na yote yanayohusu fani ya udaktari katika taifa letu,” alisema Dk Mkopi.
Dk Mkopi aliwataka viongozi wa wizara na taasisi kuacha kutumia lugha za vitisho wakati kama huu hasa baada ya kushindwa kuwalipa madaktari stahili zao.
Alisema wamesikitishwa na migogoro na migomo inayoendelea katika hospitali mbalimbali nchini kwa madaktari wanaofanya kazi chini ya usimamizi ‘Interns’ na kwamba, Serikali haijawalipa malipo yao kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi mitatu.
Dk Mkopi alifafanua kwamba hali hiyo imewafanya washindwe kuendelea na kazi yao ya kuokoa maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.
“Ikumbukwe kwamba madaktari hawa walio chini ya uangalizi ndiyo uti wa mgongo wa utoaji huduma katika hospitali wanazofanya kazi, hasa ikichukuliwa kuwa wao ndiyo wa kwanza kumwona mgonjwa na kumpa matibabu kabla ya kuonwa na madaktari bingwa walio wachache,” alisema Dk Mkopi.
Aliongeza kwamba baada ya kufanya utafiti wa kina, chama hicho kimebaini kuwa hospitali tano za rufaa nchini tayari madaktari hao wameshindwa kufanya kazi kutokana na kutolipwa fedha zao.Dk Mkopi alizitaja hospitali hizo kwamba ni pamoja na ile ya Muhimbili, Hospitali ya Bombo, Tanga; Mount Meru Arusha, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Manispaa ya Temeke.
Katika maeneo ambayo madaktari wanaendelea kufanya kazi alisema imebainika ni kutokana na vituo, hospitali au halmashauri husika kuamua kuwakopesha wataalamu hao ili kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kila siku huku wakitoa huduma wakati ufuatiliaji ukiendelea kwenye Serikali Kuu.
Chama hicho pia kimebaini kuwa hali hiyo inaenea katika hospitali nyingine zenye madaktari na inaleta mzigo kwa madaktari bingwa na waandamizi na kuonya kuwa inaweza kuleta mgogoro katika fani yote ya udaktari nchi nzima.“Chama kinatafsiri kitendo cha kutowalipa madaktari malipo yao na kuwafanya waishi kwa shida kwa muda huo wote kuwa ni kitendo cha dharau kwa fani ya udaktari na huduma wanazotoa kwa wananchi,” alisema na kuongeza:
“Pia ni udhalilishaji wa hali ya juu kuwaacha madaktari waishi kwa kuombaomba huku wakitoa huduma kwa wananchi. Ni jinsi gani Serikali isivyojali huduma za afya kwa wananchi inaowaongoza.”
Alisema chama kinalaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kutowalipa madaktari malipo yao halali hadi kufikia mgomo unaowafanya wananchi kukosa huduma stahili za matibabu.
Dk Mkopi aliitaka jamii na Serikali ielewe wazi kuwa madaktari kuwepo kazini bila malipo kwa muda mrefu ni uvunjifu wa haki za binadamu, kinyume na kiapo cha udaktari na kusababisha utoaji wa huduma hafifu na vitendo vya uvunjifu wa sheria kama kukaribisha mazingira ya rushwa.
Alisema sehemu ya kiapo cha udaktari inayozungumziwa inasema: “Wakati nikishika kiapo na ijaliwe kwangu kufurahia maisha na kazi yangu, jamii inikumbuke na kuniheshimu nikiwa hai au nimekufa.”
Alisema wanapinga unyanyasaji unaofanywa na wizara kwa wataalamu wake na kwamba Serikali iwe na mipango endelevu na ya muda mrefu katika kulipa stahili za wafanyakazi ili kuepuka kufanya kazi kwa zimamoto kama inavyofanya sasa. Dk Mkopi alisema chama kinaona wataalamu hao hawana hatia ya uvunjifu wa kiapo chao katika kutoa huduma kwa Watanzania kutokana na Serikali kutokutimiza wajibu wake kama inavyoelezeka kwenye kiapo na makubaliano ya kazi.
Hata hivyo, alisema wanasikitishwa na matokeo yanayotokana na mgogoro huo kwa wananchi wasio na hatia na taifa kwa ujumla na kuzipongeza hospitali na halmashauri zilizoamua kuwalipa malipo yao ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.
Mgomo Muhimbili
Kwa upande wa Muhimbili, hali bado ni tete baada ya madaktari wanafunzi kuendeleza mgomo wao kushinikiza Serikali iwalipe posho zao. Mgomo huo ulioanza juzi unahusisha madaktari 229 katika kada za tiba ya vinywa, wafamasia, maabara na dawa ambao wanaidai zaidi ya Sh176 milioni.
Jana katika hospitali hiyo kulikuwa na kundi kubwa la madaktari hao wakiwa wamekaa katika jengo lao huku wengine wakiwa wamejikusanya katika makundi tofauti.
Mmoja wa viongozi wa madaktari hao, Jackson Nyabusani alisema hadi jana malipo yao yalikuwa hayajafanyika kama ambavyo Serikali iliahidi.
Ahadi ya Dk Mtasiwa
Juzi, Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mutasiwa aliwaahidi madaktari hao kuwa posho hizo zingeanza kulipwa jana na kwamba zilichelewa kutokana na taratibu za Serikali katika malipo.
“Tuliahidiwa leo (jana) tungeanza kulipwa posho zetu lakini hadi sasa hakuna kitu, kila nikienda kwa mhasibu mkuu ananiambia bado,” alisema Nyabusani.
Alisema suala hilo licha ya kuwaathiri wao, pia linawaathiri wagonjwa kwani kwa kiasi kikubwa madaktari wanafunzi ndiyo wanaotoa huduma katika hospitali hiyo.
Alisema idadi kubwa ya madaktari hao wametoka mikoani huku wengine wakiwa na familia zao na kwamba wanategemea posho hizo kwa ajili ya kutafuta makazi pamoja na gharama nyinginezo.
Kiongozi huyo alisema kati ya madaktari wanafunzi 229 wanaohudumia hospitalini hapo, madaktari 50 tu ndiyo wanaokaa katika hosteli zilizopo hospitalini hapo na wengine wanaishi mitaani

Mwananchi
1 comment:
Shame on those who are responsible in causing hardship to these doctors. whoever is directly and/ indirectly they should be releaved from their duties.How do you expect these doctors to pay for food,rent,transport if they are not paid on time??? This is a systemic problem especially in Tanzania.There is need to find root cause and fix it. We have seen these kinds of injustice frequently especially in ministries of health and higher education.Mr president you should take tough measures to avoid further chaos.
Post a Comment