Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imesema kuwa kuanzia leo hadi Januari 10, mwaka huu mgandamizo mdogo wa hewa katika katika eneo la rasi ya Msumbiji unaoendelea kuimarika hivyo kusa ongezeko la mawingu katika maeneo ya kusini mwa nchi.
Taarifa ya TMA ilisema hali hiyo itaendelea kuimarisha makutano ya upepo wenye unyevu nyevu katika maeneo hayo hivyo kusababisha vipindi vya mvua kubwa katiia maeneo ya nyanda za Juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa); maeneo ya kusini mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara) na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani na kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge).
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkirugenzi Mkuu, Dk. Agnes Kijazi, ilieleza kuwa aidha, mvua za kawaida za masika zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo ya kanda ya kati (mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (mikoa ya Kigoma na Tabora).
Dk. Kijazi alisema maeneo ya Pwani ya kaskazini (mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwa vya unguja na Pemba), baadhi ya maeneo ya kanda ya kati (mikoa ya Singida, Dodoma) na baadhi ya maeneo ya kanda ya nyanda za juu kaskazini mashariki yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua ambazo ziko nje ya msimu.
“Mvua hizi zinatarajiwa kuambatana na upepo mkali katika maeneo ya Bahari ya Hindi, hivyo watumiaji wa Bahari wanatakiwa kuchukua tahadhari,” alisema Dk Kijazi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment