ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 5, 2012

WAMACHINGA JIJINI MBEYA WAENDELEA KUJIMILIKISHA BARABARA

Baadhi ya wamachinga wa jijini mbeya wanaendelea kujimilikisha baadhi ya barabara za mwanjelwa na makunguru huku halamashauri ya jiji ikiwatimaza kwa jicho la uchu isijuwe la kufanya mpaka sasa jiji halijatenga eneo maalumu la kufanyia biashara wamachinga hao


Pamoja na Jitihada za kuhamasisha wafanyabiashara ndogo ndogo kuwa na maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao bado Halmashauri ya Jiji la Mbeya haijabuni mbinu mbadala kwa ajili ya kuwasaidia Machinga kuwa na eneo maalumu la kufanyia biashara, hata hivyo wafanyabiashara hao wanadai kuwa aina ya biashara wazifanyazo ni za kuwafuata wateja kule waliko huku wakizunguka na biashara zao mitaani,

wamachinga wakifurahia kuruhusiwa kufanya biashara maeneo waliyokatazwa
(picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog)

No comments: