ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 19, 2012

Shukrani kwa waTanzania wa DMV kutoka kwa Raisi Iddi Sandaly.


Iddi Sandaly-Rais Jumuiya Watanzania DMV

Nachukua fursa hii kuwashukuru rasmi kwa uchaguzi wa April 15 ambao umetupatia uongozi katika Jumuiya yetu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka mitano. Kwa hakika ushindi si kwa viongozi waliochaguliwa isipokuwa ni ushindi kwa Jumuiya yenyewe. Tulipo leo sio tulipokuwa April 14. Kwa pamoja tumeonyesha nia ya kuunganisha nguvu zetu rasmi na kuleta umoja ambao utasaidia katika maslahi yetu wote kijamii pamoja na taifa letu tunalolipenda– Tanzania.

Sisi mliotuchagua kuongoza juhudi hizo tuna jukumu la kuhakikisha tunatetea, kusikiliza na kuendeleza haki na maslahi ya kila mtanzania. Moyo tulioonyesha katika uchaguzi huu uendelee kuwa chachu ya kuhakikisha tunafanya kazi kwa pamoja, kuinua Jumuiya yetu mpaka pale ambapo tunadhani inastahili kuwepo.

Kama tulikwaruzana katika mchakato huu basi tusameehane, tusirudie makosa na tuangalie mbele kama Jumuiya yenye umoja, upendo na ustahimilivu.

Maana halisi ya Demokrasia iliyokomaa ni kwamba baada ya uchaguzi kwisha Kazi na kipindi muhimu cha kufanya kazi kwa pamoja kinaanza.

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu ibariki Jumuiya DMV

Wenu ,
Rais,

Iddi Sandaly

No comments: