Sisi kama watanzania
tumefarijika sana na juhudi ambazo raisi Jakaya kikwete na serikali yake
amefikia.Miongoni mwa mafanikio hayo ni serikali kuweka mipango madhubuti
katika sekta ya kilimo.Kutokana na takwimu za world bank zinaonyesha mpaka sasa
nchi ya Tanzania imeweza kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 96%,
ukilinganishwa na nchi nyingine yeyote barani Afrika. Hili imelipelekea taifa
letu la Tanzania kupewa heshima kubwa Na viongozi wa G8 summit na kuwa mgeni
katika mkutano huo camp David Maryland.
Watanzania tunaamini
kwamba matumaini mapya ya kuendeleza uchumi wa nchi ni kuwasogeza wananchi
katika jitihada za kuchangia uchumi wa nchi yao.
Miongoni mwa ajenda
kubwa za mkutano huo ( G8 summit) ni kwa jinsi gani mataifa matajiri na ambayo
yanauwezo wa kiuchumi kuweza kuzisaidia nchi za afrika kukabiliana na wimbi la
uhaba wa chakula na lishe kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Ukweli
unafaamika namna gani nchi hizi zinavyokabiliwa na changamoto hizo. Vile vile
kutokana na taarifa iliyowasilishwa katika summit ni ile ambayo ilitolewa na
The future of world food and nutrition security ambayo ilisema” Sekta ya kilimo
inaendelea kuongeza GDP mara nne katika nchi nyingi duniani kuliko sekta
nyingine kwa sasa”.Huu ulikuwa ujumbe ambao ulitolewa na rais wa IFAD (
International Fund for Agriculture
Development) alisema” Small farmer as a group are the largest private
investors in African agriculture and supporting them to be more profitable must
be a key goal of the newest effort to help countries in the region tackle food
security and economic development challenge”. Naye raisi wa Marekani, President
obama alisema, “we can unleash the change that reduces hunger and malnutrition
we can spark the kind of economic growth that lift people and nations out of
poverty”. This is new commitment we are making”.
Mafanikio
yaliyopatikana na mkutano huo ni nchi yetu kuweza kupata msaada wa takribani
dola za kimarekani milioni 900. Watanzania juhudi na hatua ambazo serikali
imeonyesha na kuchukua zimeunda mazingira mapya ya Tanzania kwa kurekebisha
uchumi wa taifa, na kuimarisha menejimenti ya uchumi huo. Hilo limepelekea
wahisani wamelazimika kurudisha ushirikiano wao wa Tanzania wa misaada ya
kifedha. Hii ni mipango imara na madhubuti ya raisi Jakaya kikwete katika sekta
ya kilimo na kuifanya nchi itambulike na kupata heshima kubwa duniani ya kuwa
mfano wa kuigwa na nchi nyingine barani Afrika kwa kuwa uongozi makini na
unaowajibika. Ndiyo maana Tanzania imepewa sifa za kuigwa katika mpango huo wa
kukabiliana na huaba wa chakula na lishe barani afrika. Sisi kama watanzania tuna matumaini makubwa
na serikali kwa fedha za msaada zitaboresha sekta hii ya kilimo. Tunamatumaini
makubwa serikali itaongeza idadi ya wataalamu bora katika sekta ya kilimo,
mbegu bora na zakutosha, Kuboresha ardhi rutuba, kuwapatia wakulima wadogo
wadogo zana za kisasa za kilimo, kujiimarisha katika sekta ya umwagiliaji
badala ya mvua na kupata wataalamu wa sayansi na teknologia, kujenga vituo vyo
utafiti wa kilimo cha kisasa na kuboresha vile vilivyopo. Mpango huu utaisaidia
serikali kutoa ajira kwa vijana wengi katika sekta ya kilimo kwa kuwapa semina
na mafunzo ya kilimo bora cha kisasa na serikali kutoa vipunguzo vya kodi ya
waingizaji wa zana za kilimo nchini.Vile vile serikali itaweza kuwasaidia
wakulima kuboresha bidhaa zetu katika ushindani wa kibiashara nje ya nchi. La
mwisho sekta hii itatoa fursa mpya kwa watanzania kuweza kulisha nchi jirani
kama vile Kenya, Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi na south Sudan.
Mwisho, tunampongea
raisi jakaya kikwete kwa kuweza kuwa na
mipango madhubuti katika sekta hii ya kilimo na kulipatia taifa heshima kubwa
katika bara la afrika.Vile vile msaada huu kutoka nchi tajiri duniani ni
mafanikio ya kuweza kupata nafasi nyingine kukabiliana na changamoto zilizopo
katika kilimo. Sisi watanzania tumefarijika kwa hilo.
Mungu ibariki afrika
Mungu ibariki Tanzania
Kinyemi
Washington DC
2 comments:
very nice kinyemi katibu wa ccm!!
Kaka kinyemi Rejea Kitabu cha William Easterly(2006) , kiitwacho “Mzigo wa Mtu Mweupe”( White Man’s Burden)
Kitabu hiki kinaonesha kwa miaka zaidi ya 50 wazungu wamekuwa wakipeleka misaada Afrika zaidi ya $ 2.3 trilion dola-bado umaskini, rushwa, na Janga la UKIMWI linandelea kuwa suala zito. Misaada ya nje inasababisha matatizo kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania. Jambo muhimu kwa nchi zilizoendelea kama kweli wanataka wasaidie AFRICA ni Kuiacha Africa ijiendeshe yenyewe.
Naona mafanikio uliyoyaona kwa Rais wetu ni Msaada wa Million 900! What a shame , Kupewa Misaada ni Mafanikio?
Tanzania inatakiwa ikuwe kiasili(Naturally) na sio kwa kutegemea misaada. Na ndio maana nchi za Africa zinabweteka na kuvunjika vunjika huku tukingoja watu weupe waje kuokota vipande vipande na kujenga tena. Mpaka lini ?
Nchi yetu kamwe haitajengwa kwa Misaada . Nchi yetu inahitaji vitu vifatavyo ili tuendelee na tuweze kujikomboa kiuchumi au kiafya if you like.
1. Uhuru wa vyombo vya Habari
2. Uhuru wa Bank Kuu
3. Uhuru wa Mahakama
4. Nutral and Professional armed forces
5. Ufanishi kwa Watumishi wa Uma.
6. Tume Huru ya Uchaguzi
Kama Muheshima Kikwete au Kiongozi mwengine anaweza kuhakikisha vitu hivi sita vinafanyika bila serikali kutia DOMO/KONO lake basi Tanzania itafika pazuri tu.
Hata wazungu nao wanalalamika kuwa misaada mingi inaishia kwenye mikono ya Viongozi waovu wa Tanzania, hatimae baada ya kusaidi watu inaishia kutumiwa na viongozi hao wachache kukaa na kungangania nafasi zao za kisiasa.
Tatizo la Misaada ni kama Vile wazungu wanadhani wanajuwa Matatizo yetu, kwa hiyo basi wanatupa pesa tuyatatue. Misaada ni sawa na mtu kutoka nje kumwambia mwenye nyumba jinsi ya kutatua matatizo yake ya nyumba. Misaada haisaidii bali inabomoa , Watanzania tulijue hili. Unapewa misaada ili uwe kibaraka na sio ili uendelee au uwe huru.
Bwana William Easterly, profesa katika chuo kiku cha New york alisema
“Marekani ishatumia Dola Billion 600, katika kipindi cha miaka 45, iliyopita, na baada ya yote haya mtoto wa Africa bado anashindwa kupewa msaada wa dawa yenye gharama ya 12-cents($0.12) ya kutibu Malaria. Na kulikuwa na vifo vya watoto million 3, mwaka jana kutokana na Malaria. Pesa zinazokwenda Africa aziwafikii walengwa bali zinaishia kwa mafisadi na hatujafanikiwa kuongeza kiwango chao cha maisha hata kwa asililimia 1”
Napenda kusema kwamba Watanzania tunacho taka ni haya matatu-
1. Reform
2. Reform
3. Reform
Mungu Ibariki Tanzania.
Post a Comment