ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 24, 2012

Wanawake ni chanzo cha matatizo ya nguvu za kiume



WIKI hii mpenzi msomaji wangu nitazungumzia tatizo la nguvu za kiume ambalo limekuwa likiwasumbua wanaume wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida.
Hii imesababisha baadhi yao kuhangaika huku na kule kutafuta dawa na hata wanapofanikiwa wanajikuta wakiendelea kuwa na tatizo hilo. 

Kwa kifupi ni tatizo linalozisumbua ndoa nyingi kwani mwanaume yeyote anayejijua ni rijali anapokumbwa na tatizo hili hukosa hali ya kujiamini na kumfanya asiwe na amani na wakati mwingine kuhisi hastahili kuwa na mke.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa makala za ndoa na uhusiano utabaini kuwa, tatizo la nguvu za kiume limekuwa likielezwa kuwa linasababishwa kwa kiasi kikubwa na vyakula tunavyokula lakini uchunguzi umebaini kuwa, wanawake wanachangia kwa kiasi kikubwa katika hili.
Mwandishi mmoja wa habari za kijamii wa Uingereza, Johnson Fredrick aliwahi kueleza kwa kina kwamba wanawake wamekuwa chanzo kikubwa cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume kama ifuatavyo:
Karaha za mwanamke
Anaeleza kuwa, karaha za wanawake kwa waume zao ni chanzo kikubwa sana cha upungufu wa nguvu za kiume. Kama mwanamke atakuwa si mstaarabu kwa mumewe na akawa ni mtu wa kuropoka lolote linalomjia kinywani mwake bila kuwa na staha, humfanya mumewe kuingiza akilini mwake kitu ambacho humuathiri watakapokuja kukutana faragha.
Chukua mfano kwamba, mwanamke anatibuana na mumewe kisha anambwatukia kwa kumwambia; ‘we mwanaume gani… huna lolote wewe ni mwanaume suruali tu.’
Maneno kama haya hayawezi kumfurahisha mwanaume na akiyaweka akilini mwake hata siku akija kukutana na mkewe kwenye uwanja wao wa kujidai kisha yakamjia, ni vigumu sana kupata ile nguvu na msisimko wa kufanya tendo kwa ufasaha.
Ndiyo maana utashangaa mwanaume aliyekutana na hali hiyo atakapojaribu kutoka nje ya ndoa yake na kwenda ‘kuduu’ na mwanamke mwingine, anaweza kuwa na nguvu za ajabu na kujikuta akilifurahia tendo tofauti na na inavyokuwa kwa mkewe.
Usaliti
Mtaalam huyo wa masuala ya mapenzi anaeleza kuwa, mwanamke ambaye ‘hajatulia’ ni rahisi sana kumfanya mume wake kukosa nguvu za kiume. Hii inakujaje? Hakuna kitu kinachouma kama kuibiwa penzi lako na mwanamke anapokuwa mrahisi wa kusaliti humfanya mumewe kuumia moyoni na hatimaye kukosa msisimko katika tendo la ndoa.
Kukosekana utundu na ubunifu
Ukijaribu kufuatilia kwa makini utagundua baadhi ya wanawake walio kwenye uhusiano, hasa ndoa si watundu na hawana ubunifu wawapo faragha na wapenzi wao. Tabia hii humfanya mwanaume awe mhimili wa pekee katika zoezi zima na pale atakapochoka hawezi kupata sapoti kutoka kwa mwenza wake, matokeo yake ni mchezo kuishia hapo.
Lakini endapo mwanamke naye anayajua mambo, atakuwa na uwezo wa ‘kumbusti’ mpenzi wake na hatimaye kufika pale walipotarajia.
Tambo zisizofaa
Kuna wanawake ambao hutumia lugha za kujitamba sana kabla ya kukutana faragha na waume zao bila kujua madhara ya baadaye. Unakuta mwanamke anamwambia mumewe maneno haya:
‘Baby leo ukirudi nitakupa mambo adimu ambayo huwezi kuyapata kwingine, wewe jiandae kwa libeneke maana ngoma ya leo haitakuwa na simile’.
Unaweza kumwambia maneno hayo mumeo kwa nia njema tu ili kumfanya arudi mapema kuwahi hivyo vinono ulivyomuandalia lakini kisaikolojia huleta mazingira ya hofu ambayo yanaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke kutokuwa nadhifu
Kuna msemo huko uswahilini usemao; mwanamke ni mazingira. Siyo uongo! Mwanamke anatakiwa kuwa msafi wa mwili na nguo hasa pale anapokuwa karibu na mpenzi wake.
Kisaikolojia mwanamke msafi ni rahisi sana kumshawishi mume wake kukutana naye faragha na hata wanapokuwa wanafanya mambo yao, msisimko huwa mkubwa.
Lakini endapo mwanamke atakuwa hajijali, anaweza kumsababishia mume wake matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Hakuna asiyefahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.
Kwa hiyo usafi wa mwili na nguo kwa mwanamke ni muhimu sana ili kuweza kuboresha maisha ya kimapenzi.
Kwa leo nilidhamiria kuwaandikia hayo nikiamini ukiyafanyia kazi yatakuwa ni yenye manufaa kwako na mpenzi wako.
Tukutane wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

MBoth sides. Hapo mwandishi umekosea kidogo, Kila mtu ana feelings kama mwingine jamani.