Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, amewashambulia wakuu wa mikoa waliokuja kusikiliza bajeti ya Ofisi wa Waziri Mkuu, na kudai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali na wamekuja kula kiyoyozi bungeni.
Akichangia bajeti hiyo jana, Wenje alisema wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa wamekuja na magari ambayo wanawekewa mafuta na wanapewa posho za kujikimu wakiwa Dodoma.
Alisema matumizi ya serikali bado ni tatizo na kwamba wakuu hao wa mikoa na makatibu tawala wamefika mkoani hapa tangu Jumamosi wiki iliyopita.
Alihoji kuwa wamekuja kufanya nini bungeni ama wamekuja kula viyoyozi katika sehemu ya Spika.
“Si hao tu; watakuja watu wa wizara ya ujenzi, watakuja watu wizara…wanakuja kufanya nini hapa? Wameacha kazi mikoani mwao, jaribuni kubadili mbinu hizi jamani,” alisema.
Wakati Wenje aliwalipua wakuu hao wa mikoa, kamera iliwaonyesha baadhi yao waliokuwa kwenye jukwaa la wageni wakionyesha mshangao kwa kauli hiyo, pia aliongeza makali yake kwa kusema kuwa kuna mwekezaji ambaye ameshindikana nchini kwa kuwa na paspoti kadhaa za nchi mbalimbali, na kufanya vitendo vingi vya kuvunja sheria, lakini bado yuko nchini.
“Huyu mtu sijui ni raia wa nchi gani, ana paspoti za tatu za Burundi za Kenya… alifukuzwa nchini wakati Mheshimiwa Nohodha (Shamsi) akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, lakini muda si mrefu akarudi nchini, hata Waziri hakuwa na habari,” alisema akichangia mjadala wa hotuba ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema mwekezaji huyo amefanya makosa mengi, ikiwa ni pamoja na kuwatukana na kuwapuuza viongozi wa serikali akiwamo aliyekuwa Kamsishna wa Madini, Dadley Kafumu na Mkurugenzi wa Madini kanda ya Ziwa.
Wenje alisema mwekezaji huyo ni yule yule aliyetajwa na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Muhammad, kuwa ameshindikana.
Wenje aliwasilisha vielelezo mezani kwa Spika kutaka mwekezaji huyo aliysema ni jeuri ashughulikiwe.
Aidha, alisema kuna watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambao walitafuna Sh. bilioni mbili na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliunda tume kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo.
Alisema ubadhirifu huo uligunduliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuhoji iweje iundwe tume kuchunguza jambo hilo ikiwa tayari wataalamu walimeshasema kuwa fedha hizo zimeibiwa.
“Hakuna haja ya kuundwa tume tena, mheshimiwa waziri mkuu kamateni watu wapelekeni mahakamani kieleweke,” alisema.
Pia alizungumzia kuhusiana na sifa zilizotolewa kuwa Rais Jakaya Kikwete kwamba alishawishi mkutano wa nchi tajiri duniani na Tanzania ikapatiwa msaada wa Sh. trilioni 1.4.
Alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika bajeti yake alisifia safari za rais zina tija kwa kutolea mfano wa msaada huo uliopatikana kutokana na safari zake.
Alihoji nini cha kujivunia katika jambo hilo wakati ni jambo la aibu kupewa msaada.
Huku akirudia mara kwa mara neno aibu, Wenje alisema jambo la kujivunia ni kukusanya mapato kwa nchi na siyo kupata misaada.
Aidha, alizungumzia kuhusiana na ukubwa wa baraza la mawaziri ambalo alidai licha ya Rais kuunda upya baraza hilo bado ni kubwa.
Alisema baraza hilo lina mawaziri 57 wakati nchi zilizoendelea kama Uingereza, Italia, Ufaransa na Marekani ambayo zina baraza la mawaziri dogo.
Alihoji kiburi cha kuunda baraza kubwa la mawaziri kinapatikana wapi.
Kuhusu bei ya pamba, alisema anaungana na wabunge wenzake wa mikoa inayolima zao hilo kwamba wakulima hawatauza kama kilo moja haitafikia Sh. 1,000.
Hali kadhalika, alitaka wavuvi wa samaki ambao wanategemea kwa kiasi kikubwa shughuli hiyo katika maisha yao ya kila siku, watengewe ruzuku ambayo itawafidia kila inapotokea kushuka kwa bei.
Alisema wavuvi wengine wamepata mikopo kutoka taasisi za fedha na hivyo watashindwa kulipa madeni kwasababu watafilisika.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment