Saturday, July 14, 2012

DR SLAA AJISALIMISHA POLICE

Hata hivyo, baada ya kuripoti Dk Slaa aligoma kuandikisha maelezo ya tuhuma alizotoa hivi karibuni kwamba kuna njama zimepangwa kuwaua viongozi waandamizi wa Chadema akiwamo yeye mwenyewe.
Hatua aliyochukua jana Dk Slaa ni tofauti na aliyotoa siku chache zilizopita baada ya kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuagiza kwamba lazima viongozi hao wa Chadema wahojiwe na polisi kutokana na madai yao kuwa wanataka kuuawa na mmoja wa kigogo wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Baada ya agizo hilo la Waziri Nchimbi, Dk Slaa alisema hatakwenda polisi, wakitaka polisi wakamkamate.
Alilitaka jeshi hilo litumie taarifa zake za kiintelejensia kubaini watuhumiwa waliowataja katika mkutano wa waandishi wa habari hivi karibuni.
Dk Slaa; "Kwani wao wanapozuia mikutano yetu kwa madai kwamba taarifa zao za kiintelejensia zinaonyesha kutakuwa na vurugu huwa tunauliza wamezitoa wapi?"

No comments: