Juu na chini ni Watanzania wa Massachusetts na majimbo ya jirani waliofika katika Sala ya Ijumaa katika msikiti wa Roxbury uliopo Barabara ya Malcolm X Blvd, Roxbury, Massachusetts Nchini Marekani.
Mzam "Chadogi" rafiki wa karibu na marehemu akiangalia mahali atakapozikwa Patrin Kibelloh
Gari liliobeba mwili wa marehemu likiwasili makaburi ya West Roxbury yaliyopo mtaa wa Baker alikozikwa Patrin Kibelloh
Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki waliofika makaburini kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho wakisaidiana kubeba jeneza kuelekea mahali atakapozikwa marehemu.
Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki wakisaidiana kufukia mahali alipozikwa ndugu yetu Patrin Kibelloh.
Baada ya maziko viongozi wa jumuiya ya Watanzania New York na Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Massachusetts wakipiga picha ya pamoja.
Mke wa marehemu Iman Mwakawago (wapili toka kulia waliokaa) akiwa pamoja na ndugu, marafiki na jamaa wakimfariji katika msiba huu mkubwa.
Maftaha kutoka New York akiongea machache katika kuwafariji wafiwa
Isaac Kibodya akitoa shukrani kwa niaba ya familia
Kwa picha zaidi Bofya Read More
11 comments:
mungu awajalie kwa kufanikisha kumzika mwenzetu,huu ni upendo na moyo wa kitanzania
shukulani kwa ndugu wote mlio weza kumzika kaka yetu Pat mwenyezi hamzudishie huzima wa milele tutaku miss BABU KUBWA
R.I.P marehemu
RIP brother
bwana ametoa bwana ametwaa poleni wafiwa.
Pumzika kwa amani kaka yetu. Poleni wote.
R.I.P Pat.
One thing about Tanzanians is the Highest Respect they show when one member of the Community goes down!!!
Bravo!!! Keep that UP !!!
Mdau,
NC
Nilipata habari ya kuzikwa ndugu yetu ila nimesikitishwa na waislamu waliohusika kuwaruhusu wanawake kwenda makaburini na ilhali sio katika uislamu na imekatakazwa sijui ni uislamu in western unapokwenda na wakati ama wana ushahidi upo wa kuwaruhusu wanawake kushiriki makaburini wanawake basi nimeonelea kuwapa kipande hiki cha ushahidi wa uislamu ili isidiriki katika umma wa kiislamu siku nyingine na inshallah mungu uwe wenye kutuongoza isitokee siku nyingine.......
Kama tunavyokariri kusema kuwa Uislamu ni njia kamili ya maisha ya mwanadamu akiwa hapa duniani. Na miongoni mwa agizo ni la kufuata jeneza kwa wanaume. Katika Uislamu, mwanaume na mwanamke wanasaidia katika kutekeleza majukumu. Hivyo, katika suala hili wanaume wameruhusiwa kufuata jeneza mpaka makaburini na wanawake wamekatazwa. Katazo hilo ni kulingana na Hadiyth ya Ummu ‘Atwiyyah (Radhiya Allaahu ‘Anha) ambaye amesema: “Tumekatazwa kufuata jeneza” (al-Bukhaariy na Muslim). Hakika ni kuwa wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hawakuwa ni wenye kufuata jeneza.
Hivyo kufuata agizo la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni wajibu wetu kwa kauli ya Aliyetukuka: “Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho” (59: 7).
kwizeraster@gmail.com
WEwe au nyie mliotoa komenti,sijui ni mmetoa kuonekana kwenye vijimambo au mnaju a dini sanaaa!mimi ni muislamu halisi na ninajua sheria,lakini tafadhali kabla hujasoma ukaona picha na ushahidi usiandike kitu usichokijua,kwa taarifa yako "WANAWAKE" hawakuwepo,walikuwepo kwa kuombea na nyumbani kwa marehemu tuuu!mimi ni muislamu,mwanaume na nilikuwepo mazikoni na makaburini tulikuwa wanaume tuuuu!sasa sijui wewe umetoa wapi haya,huo ni uzushi na ufitinishi mkubwa!!angalia maelezo na picha vizuri na kwa makini ndugu MUISLAM wewe/nyie watoa/mtoa mada.Tafadhali naomba itolewa tamko rasmi kwa wahusika au ndugu/jamaa wa karibu wa marehehemu ili kuliweka sawa jambo hili maana hii inasomwa duniani kote na watanzania wote wataelewa vibaya na kuweka rekodi mbaya kwa waislamu tunaoishi huku kwa ajili ya watu kama hawa wanaoongea vitu wasivyokua na uhakika navyo>Inshallah tunakushukuru sana DJ LUKE mzeee wa Vijimambo kwa kutuunganisha watz wote duniani kwa blog yako,asante sana na mnyaazi mungu atakujalia.Asante sana.
Post a Comment