Aidha Balozi huyo amesema katika kipindi cha miaka tisa toka 2003 watu wa Marekani kupitia PEPFAR wamewekeza dola za Kimarekani Bilioni 2 kwa ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI nchini Tanzania ambao ni uwekezaji katika maisha.
Kwa
mujibu wa taarifa ya mapambano dhidi ya Ukimwi Mkoani Iringa kwa
kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo Iringa imeathirika kwa kiwango
kikubwa ukilinganisha na Mikoa mingine Tanzania ambapo utafiti
unaonyesha maambukizi ya VVU na janga la UKIMWI kitaifa uliofanyika
mwaka 2007/2008 maambukizo yameongezeka kutoka asilimia 13.4% mwaka
2003/2004 na kufikia asilimia 15.7.
Aidha
hatua ya mkakati huo imewezesha Watanzania zaidi ya 300,000 kutumia
dawa zinazopunguza makali ya VVU ambapo hivi sasa zaidi ya Watanzania
525,000 hupokea matunzo na huduma mbalimbali zikiwemo huduma za
majumbani.Habari na Picha na Gustav Chahe
No comments:
Post a Comment