MtendajiwaTAMWA anayemaliza muda wake,Ananilea Nkya
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)
kimepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambaye anachukua nafasi ya Ananilea
Nkya anayemaliza muda wake baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka
11.
Mkurugenzi huyo mpya wa TAMWA, Valerie Msoka ambaye ni miongoni mwa
wanahabari wanawake 12 walioanzisha TAMWA, amefanya kazi za kutukuka
katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Valerie Msoka
atakabidhiwa rasmi ofisi Alhamisi tarehe 27 Septemba katika sherehe fupi
itakayofanyika kuanzia saa 3.30 hadi ya 5.00 asubuhi.
Sherehe hiyo itakayofanyika katika ofisi za TAMWA zilizoko eneo la
Sinza-Mori, Dar es Salaam inatarajiwa kuhudhuriwa na wahariri na
wanahabari kutoka vyombo vya habari mbalimbali, wawakilishi wa mashirika
ya wanahabari, Wakurugenzi Watendaji kutoka mashirika ya kiraia na
viongozi wa TAMWA wa zamani na sasa.
Valerie Msoka alifanya kazi Radio Tanzania Dar es Salaam, shirika la
utangazaji la Uingereza BBC idhaa ya Kiswahili na Kiingereza kabla ya
kujiunga na Umoja wa Mataifa. Kadhalika Valerie Msoka mwenye shahada ya
Uzamiri katika fani ya Uandishi wa habari wa Kimataifa (M.A in
International Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha City nchini Uingereza,
amefanya kazi kwenye maeneo ya vita ikiwemo Iraq, Sudan, Rwanda, Congo
na Burundi.
Valerie Msoka anachukua uongozi wa TAMWA wakati shirika likiwa
linajiandaa kuanza kutekeleza mradi mkubwa wenye lengo la kuimarisha
vuguvugu katika harakati za kujenga usawa wa kijinsia na kutokomeza
vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
TAMWA itatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP), Chama Cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Chama Cha
Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi (CRC).
Wilaya kumi zitanufaika na mradi huo ambazo ni Wete (Pemba
Kaskazini), Unguja Magharibi (Unguja Urban West), Wilaya ya Unguja
kusini (Unguja South district), Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara),
Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruhangwa (Mtwara), Kinondoni na
Ilala, (Dar es Salaam
Chanzo:The Habari
No comments:
Post a Comment