Amirijeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel
Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam.
Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali
Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange
(kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki
(katikati)
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni
Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto)
na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo
Ikulu jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment