Tausi Ally na James Magai
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imemwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part (DP), Mchungaji Christopher Mtikila baada kuona hana hatia kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili.Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imemwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Part (DP), Mchungaji Christopher Mtikila baada kuona hana hatia kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili.Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote hususan utetezi wa Mchungaji Mtikila na Sheria ya Magazeti, ameridhika kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha madai.
Hakimu Mugeta alisema ushahidi na vielelezo vyote vilivyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka, havielezi ni jinsi gani Mchungaji Mtikila alitenda makosa hayo.“Ninakubali kwamba mashtaka dhidi ya mshtakiwa hayakuthibitishwa na Mahakama inamwachia huru katika mashtaka yote,” alisema.
Katika hukumu hiyo, Hakimu Mugeta alisimamia zaidi maelezo yaliyomo ndani ya waraka huo badala ya ushahidi wa pande zote kutokana na Mchungaji Mtikila kukiri kuandaa, kumiliki na kusambaza waraka huo uliodaiwa kuwa ni wa uchochezi.
Hata hivyo, hakimu huyo alisema maelezo matupu yaliyomo katika waraka huo hayatoshelezi kufanya kosa la uchochezi.
Alisema kwa mujibu wa Mwongozo wa Sheria za Kiingereza, mambo yanayounda kosa la uchochezi ni vurugu, kuhamasisha vurugu, kuhamasisha usumbufu kwa jamii, kuhamasisha kutokutii na kudharau mamlaka za kisheria.
Alisema Sheria ya Magazeti, Sura ya 229 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, ambayo ndiyo upande wa mashtaka uliyoitumia kumshtaki Mchungaji Mtikila, haielezi maana ya uchochezi isipokuwa Kifungu cha 31 kinaeleza tu mambo yanayoonyesha kusudio la uchochezi.
Alisema Sheria ya Magazeti, Sura ya 229 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, ambayo ndiyo upande wa mashtaka uliyoitumia kumshtaki Mchungaji Mtikila, haielezi maana ya uchochezi isipokuwa Kifungu cha 31 kinaeleza tu mambo yanayoonyesha kusudio la uchochezi.
Alisema Kifungu cha 31 (3), kinaelezea tu namna ya kutambua kama tendo lililofanywa, neno lililotamkwa au waraka uliochapishwa ni wa uchochezi na kwamba lazima yaonyeshe matokeo ambayo yatafuata kutokana na mwenendo wa mhusika katika wakati na mazingira aliyofanya hivyo.
“Kwa mtizamo wangu, kwa kitendo, neno lililozungumzwa au waraka uliochapishwa kuwa uchochezi, lazima ufuatane na matokeo…Ni mtizamo wangu kwamba machapisho matupu tu bila matokeo ya kusababisha chuki, dharau, uchochezi wa kutokuridhika, kujaribu kusababisha mabadiliko ya jambo lolote kinyume cha sheria humaanisha kuhamisha dhamira mbaya, haiwezi kuwa uchochezi.” alisema Hakimu Mugeta.
Alisema mashtaka katika makosa yote mawili hayaelezi ni uchochezi upi uliokusudiwa katika kuchapisha waraka huo na kwamba anadhani mashtaka yalipaswa kuwa na taarifa za wazi ambazo zingemwezesha mshtakiwa kuandaa utetezi wake.
Kuhusu madai ya kumwondoa Rais Kikwete madarakani kinyume cha sheria, Hakimu Mugeta alisema ametafakari kielelezo cha kwanza ambacho ni Gazeti la Mwananchi lenye habari ya mshtakiwa kuwafundisha Wakristo kumwondoa Rais Kikwete madarakani, ni kupitia sanduku la kura.
“Kwa kifupi, mshtakiwa anawataka Wakristo wenzake kutompigia kura Rais Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,” alisema.
Alisema Kifungu cha 21 (2) (C) cha Sheria ya Magazeti, kinaeleza kuwa habari siyo ya uchochezi kwa sababu tu inakusudia kushawishi watu kufanya mabadiliko kwa njia za kisheria kama sheria zinavyoeleza.Mtikila baada ya kuachiwa huru na kuondoka kwenye Mahakama ya wazi, saa 7:05 mchana akiwa bado yupo kizimbani, alipiga kelele akisema Haleluya! Haleluya! Haleluya.
Alidai kuwa hakuona sababu ya kumweka Wakili wa kumtetea dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili, kwa sababu aliona wataharibu kesi.Hata hivyo, alisema hatafungua kesi ya madai dhidi ya Serikali, labda yenyewe ikate rufaa akisema yupo tayari kwa ajili yao.
Anusurika kutiwa mbaroni
Baada ya kuachiwa, Mchungaji Mtikila alijikuta katika mvutano mkali na polisi waliotaka kumkamata tena kwa madai ya kutishia kumuua kwa maneno, mfanyabiashara Gotham Ndunguru aliyefika mahakamani hapo akiwa na taarifa ya malalamiko ya Polisi (RB).
Baada ya kuachiwa, Mchungaji Mtikila alijikuta katika mvutano mkali na polisi waliotaka kumkamata tena kwa madai ya kutishia kumuua kwa maneno, mfanyabiashara Gotham Ndunguru aliyefika mahakamani hapo akiwa na taarifa ya malalamiko ya Polisi (RB).
Ndunguru alifika mahakamani hapo na kuwataka askari waliokuwepo kumkamata na kuwaonyesha hati ya kumkamata mtuhumiwa yenye namba RB/10482/12.Baada ya kuwaonyesha, Ndunguru alikuwa akiwahimiza Polisi hao na wenzao wa Magereza kumkamata huku akiwahoji kama wanamwogopa.
Ndunguru anamtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua kwa bunduki, kuharibu mali na kuvunja nyumba yake iliyopo eneo la Kimara, Kinondoni.
Hata hivyo, polisi alipotaka kumkamata, Mchungaji Mtikila alikuja juu akisema huwa hakamatwi hivihivi kwani anakwenda mwenyewe polisi... “Mimi Polisi huwa naitwa kwa kupigiwa simu na ninakwenda mwenyewe hata Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema analijua hilo. Huwezi kunipeleka polisi mimi.”
Wakati sakata hilo likiendelea, Mtikila naye alitoa hati ya kumkamata Ndunguru na kuwaonyesha askari hao waliotakiwa kumkamata na kuwataka wamkamate akidai kuwa ni tapeli.Alidai kuwa Ndunguru anatakiwa kukamatwa na kupelekwa Mahakama ya Mwanzo, Kimara akidai ameidharau kwa kutohudhuria kesi yake.
Machi 14, mwaka huu, Mtikila alipatikana na kesi ya kujibu kwa kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Kikwete, uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo ikiwa ni siku chache baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake baada ya kuwaleta mashahidi watano.
Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa Jamhuri, amefikia uamuzi wa kumwona Mtikila ana kesi ya kujibu na hivyo kutakiwa kupanda kizimbani Aprili 11, mwaka huu kuanza kujitetea.
Februari, mwaka huu, Mtikila alikiri maelezo aliyochukuliwa na ofisa wa polisi kuwa ni yake na kwamba hana pingamizi nayo na hivyo Mahakama iliyapokea kama kielezo cha upande wa Jamhuri. Katika maelezo hayo, alikiri kuwa aliuandaa waraka huo na kuusambaza lakini alisema siyo wa uchochezi ila unahusu maneno ya Mungu.
Mtikila alikiri maelezo hayo yaliyosomwa na kutolewa mahakamani kama kielelezo baada ya shahidi wa Jamhuri, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ibeleze Mrema (54) kudai kwamba Aprili 15, 2010 akiwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam aliitwa na mkuu wake wa kazi na kumpa kazi ya kumhoji Mtikila kuhusu tuhuma za kukutwa na waraka wa uchochezi na alikiri kuhusika na nyaraka hizo na kwamba alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuokoa Wakristo na alisaini waraka huo.
“...Nilipomhoji walichapisha wapi hakupenda kusema, bali alidai kuwa zilikuwa nyaraka 100,000 ambazo zilisema kwamba Rais Kikwete anaangamiza Ukristo na amekuwa jasiri kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri.”
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari, 2009 na Aprili 17, 2010 Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshtakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema ‘Kikwete kuuangamiza Ukristo, Wakristo waungane kuweka mtu Ikulu.’
Katika shtaka la pili, Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni, Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii na katika kesi hiyo alijitetea mwenyewe.
Katika shtaka la pili, Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni, Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii na katika kesi hiyo alijitetea mwenyewe.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment