ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 26, 2012

Mke wa Bill Gates kutua Arusha leo-Mwananchi

Melinda Gates
Magreth Munisi
MKE wa Tajiri Mkubwa Duniani Bill Gates, na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watu maarufu watakaohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Kilimo utakaofanyika jijini Arusha kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema mkutano huo utakaohudhuriwa na Melinda Gates ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates, utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo ambao ni Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF), utahudhuriwa pia na mawaziri wa kilimo na wakuu wa nchi nyingine za bara hili.

Ofisa Uhusiano wa AGRA Sylvia Mwichuli, alisema maandalizi yote ya mkutano huo yameshakamilika.

Watu wengine maarufu wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano pamoja na Tanzania ni  Rais wa IFAD Dk Kanayo Nwanze na  Waziri wa Kilimo wa  Nigeria  Dk  Akinwumi Adesina.

Mkutano huo ambao lengo lake ni kujadili usalama wa chakula katika bara la Afrika, utaongozwa na Rais Kikwete akishirikiana na Koffi Annan.

“Lengo ni kujadili jinsi ya kuwa na usalama wa chakula katika bara hili, katika mijadala itakayofanyika suluhisho la kuwa na usalama wa chakula litafikiwa,” alisema.

No comments: