WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewavua madaraka wakurugenzi sita wa
Halmashauri za Wilaya kwa kushindwa kusimamia rasilimali watu, fedha na
kutowajibika.
Kutokana na hatua hiyo, Waziri Mkuu Pinda amewateua
watu sita kukaimu nafasi hizo na wakurugenzi wapya 14 huku akiwahamisha
wakurugenzi 27 kutoka katika vituo vyao vya kazi kwa sababu mbalimbali.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia, alisema wakurugenzi
hao walivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia rasilimali watu na
fedha, kusababisha halmashauri kupata hati chafu na uzembe.
Aliwataja
wakurugenzi hao waliovuliwa madaraka kuwa ni Willy Njau (Mwanga),
Mpangalukela Tatala (Geita), Theonest Nyamhanga (Kishapu), Eden Munisi
(Morogoro), Mhando Senyagwa (Kyela) na Nicholaus Kileka (Ngorongoro).
Pia
alisema Serikali haitasita kuchukua hatua pale inapobidi ili kuboresha
utendaji, na kwamba wengine tayari wana kesi na si busara kuwe na mtu
anayekaimu zaidi ya miaka mitatu.
Pia alisema hatua za kinidhamu
bado zinaendelea na kwamba baadhi ya wakurugenzi hao tayari
wamewafikisha kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
kwa ajili ya hatua zaidi.
Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya
walioteuliwa kujaza nafasi hizo kuwa ni Abdalah Kidwanka (Geita),
Rutius Bilakwata (Kishapu), Naomi Nko (Magu ), Abdalah Mfaume (Kyela),
Twalib Mbasha (Monduli), Henry Ruyagu (Urambo), Adam Mgoyi (Mbarali) na
Estomih Chang’a (Mpanda).
Wamo pia Leti Shuma (Mwanga), Mohamed
Maje (Namtumbo) Fulgency Mponji (Moshi), Robert Nehata (Tunduru),
Isabela Chilumba (Kahama), Fikiri Malembeka (Sengerema), Paul Malala
(Njombe) na Nasib Mbaga (Biharamulo).
Wakurugenzi wanaohamishwa
ili kujaza vituo wazi ni Bibie Mnyamagola (Kongwa), Daudi Mayeji
(Kilindi), Protace Magayane (Nkasi), Saada Mwaruka (Mkuranga), Sipora
Liana(Tabora Manispaa), Hadija Makuwani (Wilaya ya Tabora), Doroth Rwiza
(Kasulu).
Wengine ni Kelvin Makonda (Manispaa ya Lindi),
Pudenciana Kisaka (Iringa), Tina Sekambo (Makambako), Beatrice Dominick
(Masasi), Gladyness Ndyamvuye (Bukoba), Nathan Mshana (Ngorongoro),
Cornel Ngudungi (Ngara), Mohamed Mkupete (Mtwara Manispaa), Dk Koroine
Ole Kuney (Misungwi).
Wamo pia Ephraem Ole Nguyaine (Rorya), Goody
Pamba (Igunga), Fidelis Lumato (Ludewa), Athuman (Tarime) na Ahmad
Sawa (Musoma Manispaa).
Waliohamishwa kwenda kwenye halmashauri
mpya ni Magreth Nakainga (Geita), Eliza Bwana (Bariadi), Zuberi Mbyana,
Ilemela Manispaa (Biharamulo), Mohamed Nanyanje (Masasi), Erica Musika
(Kahama), Imelda Ishuza (Busokelo).
CHANZO NIPASHE
No comments:
Post a Comment