Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
Anaitwa Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangwaka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo.
Wakazi wa mji wa Tabora wakiwa ndani ya uwannja wa Ally Hassan Mwinyi wakati tamasha la Serengeti Fiesa lilipokuwa linaondoka
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua mashine,na kulia kwake ni Hamza Balla,
Msanii Recho akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa madens wake
Pali kuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.
Mbunge wa Tabora Mjini,Mh Afeni Rage akisoma moja ya namba ya aliyebahatika kuibuka na bajaji,kulia kwake ni Mkuu wa utafiti wa Clouds .TV,Bwa.Ruge Mutahaba.
NI full mzuka mwanzo mwisho kwa mashabiki.
Hamza Balla na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
No comments:
Post a Comment