Mabingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) Yanga wako katika hatari ya kushushwa daraja au kupokonywa pointi na FIFA kutokana na kudaiwa malimbikizo ya mshahara na kocha wao wa zamani Kostadin Papic na mchezaji John Njoroge ambao kwa nyakati tofauti wameishitaki klabu hiyo kwenye shirikisho hilo la soka la kimataifa.
FIFA mapema wiki hii iliiandikia Shirikisho la Soka Nchini (TFF) barua kueleza kwamba klabu hiyo inadaiwa Dola za Marekani 12,300 (Sh. milioni 19) na Papic aliyekuwa anaifundisha timu hiyo ambaye mkataba wake ulimalizika Aprili 24 mwaka huu na kuondoka nchini mapema mwezi Mei.
FIFA tayari ilishaamuru Yanga kumlipa Mkenya, Njoroge aliyekuwa anaichezea klabu hiyo Sh. milioni 17 kama fidia kufuatia kitendo chake cha kuvunja mkataba naye na kumuacha katika muda ambao dirisha la usajili limeshafungwa.
Akizungumza jana jijini, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kuwa Yanga iko katika hatari hiyo kufuatia kutolipa madai ambayo yalishaamriwa na FIFA na sasa shirikisho hilo likiwa limepokea madai mengine yanayoihusu klabu hiyo.
Osiah alisema kuwa Yanga inatakiwa kuwasilisha vielelezo katika shirikisho hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kutokana na madai ya Papic.
Osiah alisema kuwa FIFA ina adhabu tatu kwa klabu yenye makosa ya aina hiyo ambapo ya kwanza ni kutakiwa kulipa madai yaliyowasilishwa, kushushwa daraja na kupokonywa pointi katika mechi zake za ligi ya ndani.
"Yanga inakoelekea ni kwenye kushushwa daraja au kupokonywa pointi kama ilivyowahi kufanywa moja ya klabu kubwa huko Ulaya," alieleza Osiah.
Alisema kwamba TFF haizuii klabu kuvunja mkataba na kocha au mtendaji wake ila inataka kuona taratibu za kutekeleza maamuzi hayo zinafuatwa lakini akiongeza kuwa shirikisho linasikitika kusikia klabu hiyo ya Yanga imeitimua sekretarieti yake yote kwa madai ya kutowajibika vyema.
Aliongeza kuwa tabia hiyo ya Yanga inachafua sifa ya nchi na itaiweka Tanzania kwenye mazingira magumu pale itakapokuwa kwenye mchakato wa kusaka kocha mwingine itakapomalizana na kocha wa sasa wa timu ya taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen.
YANGA WAJITETEA
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga aliliambia gazeti hili kwamba wamepokea barua hiyo ya FIFA na tayari wameshaanza kuifanyia kazi kama inavyojieleza.
Sanga alikiri Yanga kudaiwa na Papic lakini alisema kuwa kiasi anachodai ni Mserbia huyo ni kidogo tofauti na kilichoelezwa katika madai yake aliyowasilisha FIFA.
Kiongozi huyo alisema kuwa hivi sasa ndio Katibu Mkuu wao wa muda, Lawrence Mwalusako kwa kushirikiana na Katibu aliyetimuliwa, Selestine Mwesigwa wanahakiki madai ya Papic na ya Njoroge ambayo wanatakiwa kuyatolea maelezo kabla ya hatua kali hazijachukuliwa juu yao.
"Unajua kila kitu uongozi wetu umekirithi, sasa ndio tunahakiki kwanza kabla ya kuanza kujibu na kulipa madai hayo, tumeanza kujipanga kumaliza matatizo yote," alisema Sanga.
Aliongeza kwamba uongozi ulioingia madarakani utahakikisha unafanya maamuzi kwa kuzingatia vipengele vilivyoainishwa kwenye mkataba wa mchezaji au kocha ili kutorudia makosa yaliyotokea.
MBUYU TWITE
Yanga pia inatakiwa kuilipa Simba kiasi cha Dola za Marekani 32,000 (Sh. milioni 49.7) kufuatia kitendo chake cha kumsajili beki, Mbuyu Twite ambaye tayari alikuwa ameshapokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa watani zao ili kuichezea timu hiyo.
Sanga alilieleza gazeti hili kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na watatekeleza maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF kama ilivyoelekezwa.
"Suala la Mbuyu Twite bado hatujaanza kulifanyia kazi, muda bado upo," alisema kwa kifupi kiongozi huyo ambaye alichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15 mwaka huu.
Yanga ilipewa siku 21 kuilipa Simba kiasi hicho cha fedha na kuanzia Septemba 10 mwaka huu yalipotolewa maamuzi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment